Vilabu vikubwa barani ulaya vinajadili mbinu za kufanyia marekebisho ligi kuu ya mabingwa barani humo.
Muungano wa vilabu barani humo European Clubs' Association (ECA) linasema kuwalinapanga kufanya marekebisho hayo kwa ushirikiano na UEFA ifikapo mwaka wa 2018.
Kwa sasa takriban vilabu 78 vinashiriki katika ligi hiyo yenye mataifa 54.
Na baada ya mchujo wa kwanza timu 32 zinaendelea mbele na mechi za maondoano.
Baada ya mkutano baina yao wote wanaonekana kuwa na imani ya kukubaliana.
Naibu mwenyekiti wa ECA Umberto Gandini amependekeza kuwa ligi hiyo isiendelee kwa zaidi ya miezi 9 mbali na kupanga mikakati ya kufanya ligi hiyo ivutie zaidi.
ECA inawakilisha zaidi ya vilabu 200 ikiwemo Real Madrid, Barcelona, Juventus, Bayern Munich, Manchester United na Chelsea.
Kumekuwa na mapendekezo ya kutaka timu hizo kuu zifuzu moja kwa moja badala ya kufuzu kupitia mchujo wa ligi zao za nyumbani.
Mkurugenzi wa Bayern Munich Rummenigge, alinukuliwa na gazeti mojka la Ujerumani kuwa kuna mikakati ya kuzindua 'Super League''
Sheria za ligi ya mabingwa zinaizuia kufanya mabadiliko ya aina yeyote hadi baada ya kipindi cha miaka mitatu.
Awamu hii itakamilika msimu ujao wa 2017-18.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni