Ratiba
ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
imetolewa leo, ambapo jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua hiyo (16
bora) itakayoanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26-1 Machi 2015
katika viwanja mbalimbali nchini.
Michuano
hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi
Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne
huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.
Ijumaa
tarehe 26 Februari kutachezwa michezo miwili ambapo, Ndanda FC
watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar
katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi,
Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika uwanja wa
Mwadui Complex - Shinyanga, Jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza na
mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya.
Februari
28, michezo mitatu itachezwa, Simba SC watawakaribisha Singida United
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi
ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto African wakicheza
na wachimba madini wa Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Raundi
hiyo itamalizika Machi 01, 2015 kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo Young
Africans watawakaribisha JKT Mlale katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Bingwa
wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka
huu ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kombe la Shirikisho
Barani Africa (CAF CC) mwakani 2017.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni