STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 29 Februari 2016

TFF TUNATAKA DROO YA KOMBE LA FA ICHEZESHWE HADHARANI......



MICHUANO ya Kombe la FA inaingia hatua ya robo fainali na bado hatujafahamu ratiba yake iko vipi zaidi ya timu husika kufuzu hatua hiyo, ambapo bingwa ataiwakilisha Tanzania kwenye michauno ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

 


Michuano hiyo iliyorudishwa msimu huu baada ya kusimamishwa kwa miaka mingi, imeongeza ladha ya soka nchini na kila mpenda soka amekuwa akiifuatilia na kugundua nchi yetu imejaaliwa vipaji kila kona lakini vinakosa kuendelezwa. 

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndilo linahusika kwa asilimia kubwa katika michuano hii kutokana na kwamba lenyewe ndilo baba wa soka hapa nchini.

 Sijui vinatumika vigezo gani katika kupanga ratiba ya kombe hili kwani tangu kuanza kwake mpaka kufikia hatua hii, sijawahi kusikia droo ikichezeshwa kama ilivyo kwa michuano mingine kokote pale ulimwenguni. 

Ukijaribu kuuliza kwa wahusika hakuna anayekupa majibu ya kueleweka na wakati mwingine ushirikiano unakuwa mdogo. 

 Hivi karibuni dunia nzima ilishuhudia droo ya hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Europa, michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa). 
 

Cha kujiuliza hivi TFF na Uefa wanatumia sheria tofauti za soka mbali na zile zilizotungwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)? 

Sote tunajua kila michuano ina kanuni zake, lakini sheria hubaki ni zilezile, lakini katika suala hili la kuchezesha droo linapaswa kuwa ni la wazi kwa lengo la kuwaonyesha watu kuwa hakuna anayependelewa. 
 


Nasema hivyo kwa sababu nimemsikia Kocha wa JKT Mlale, Edgar Juvenary Msabila akilalamika kwamba kwa nini Yanga mechi zake za FA zote amechezea nyumbani, tofauti na timu zingine! 

Hii inaleta dhana kwamba Yanga inabebwa na TFF na wanaodhani hivyo wanakuwa na hoja thabiti kutokana na mambo yalivyo sasa. 

Lakini kama mambo yangekuwa yanafanywa hadharani sidhani kama kungekuwa na malalamiko juu ya hilo na kama yangekuwepo, basi yasingekuwa na mashiko sana. 

 Najua TFF ni chombo makini ambacho kimekuwa kikisimamia soka letu kwa weledi, hivyo itumike busara kurekebisha jambo hili ili kuwafanya watu wakiamini chombo hicho.

 Wakati mnaingia mkataba na Azam TV katika kuonyesha michuano hii, hamkujificha, kila mtu aliona jinsi mlivyoingia mkataba, lakini iweje katika ratiba kuwe na vificho kiasi hiki, kuna nini nyuma ya pazia? 
 
Nadiriki kusema makosa mmeyafanya na hamna budi kukiri, hivyo basi tunataka kuona kabla ya mechi za robo fainali hazijaanza ichezeshwe droo ambayo itahudhuriwa na watu hata kwa uchache wakiwemo waandishi wa habari kwa lengo la kuwahabarisha watu wengine waliokosa fursa hiyo.

 www.mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox