SIMBA SC imejiweka sawa kwenye mbio za ubingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga Mgambo JKT mabao 5-1 jioni
ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 39
baada ya kucheza mechi 17, sasa ikiwa inazidiwa pointi moja tu na mabingwa
watetezi, Yanga SC walio kileleni, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 39 pia.
Mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliifungia
Simba SC bao la kwanza dakika ya tano akimalizia krosi ya mshambuliaji Ibrahim
Hajib.
Kiiza akakosa penalti dakika ya 14 iliyookolewa na
kipa Mudathir Khamis, kufuatia Henry Chacha kuunawa mpira kwenye boksi
Lakini Mwinyi Kazimoto akafunga bao la pili dakika
ya 28 kwa shuti kali kutoka nje ya boksi baada ya kugongeana vizuri na Hajib.
Hajib akaenda kufunga mwenyewe bao la tatu dakika ya 42 baada ya kuwachambua mabeki watatu wa Mgambo na kipa wao Mudathir Khamis, kufuatia pasi ya Kazimoto.
Daniel Lyanga aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Hajib kipindi cha pili, aliifungia Simba SC bao la nne kwa shuti kali kutoka nje ya boksi baada ya pasi ya kiungo Said Ndemla.
Kiiza akahitimisha karamu ya mabao ya Simba SC kwa kufunga bao la tano dakika ya 82 akimalizia krosi ya Hassan Kessy, ambaye amecheza kwa kiwango cha juu leo.
Fuluzulu Maganga ‘akachafua gazeti’ kwa kuifungia Mgambo bao la kufutia machozi dakika ya 88 baada ya mabeki wa Simba SC kumuacha wakidhani ameotea.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Kessy Ramadhani, Abdi Banda, Juuko Murshid, Hassan Isihaka, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamisi Kiiza, Ibrahim Hajib/Danny Lyanga dk72 na Hija Ugando/Said Ndemla dk62.
Mgambo JKT; Mudathir Khamis, Bakari Mtama/Bolly Shaibu dk44, Salim Mlima, Salim Kipaga, Ramadhani Malima/Mussa Ngunda dk44, Henry Chacha, Sunday Magoja, Mohammed Samatta, Fully Maganga, Ally Nassor na Aziz Gilla.
Kule Mbeya
YANGA SC imezidi kupoteza matumaini ya kutetea
ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kulazimishwa
sare ya 2-2 na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Matokeo hayo hayaiondoi kileleni Yanga SC ikifikisha
pointi 40 baada ya kucheza mechi 17, mbele ya Azam FC na Simba SC wenye pointi
39 kila mmoja.
Lakini Azam FC wana viporo wawili, wakati Simba SC
ndiyo wamecheza mechi 17 kama Yanga.
Yanga SC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 35
kupitia kwa mshambuliaji wake Mrundi, Amissi Tambwe aliyefunga kichwa
akimalizia krosi ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
Prisons wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Jeremiah
Juma Mgunda aliyefunga kwa kichwa pia dakika ya 40 akimalizia krosi ya Mohammed
Mkopi.
Mkopi akaifungia Prisons bao la pili dakika ya 62
kwa kichwa pia akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa zamani wa
Yanga SC, Juma Seif ‘Kijiko’.
Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Simon
Msuva aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Deus Kaseke
aliisawazishia Yanga kwa penalti dakika ya 84 baada ya beki Meshak Suleiman kuunawa
mpira kwenye boksi.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’,
Juma Abdul, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Said Juma ‘Makapu’/Salum
Telela dk59, Deus Kaseke/Simon Msuva dk54, Haruna Niyonzima na Donald Ngoma,
Amissi Tambwe na Issoufou Boubacar.
Prisons; Benno Kakolanya, Benjami Asukile, Laurian
Mpalile, James Mwasota, Nurdin Chona, Jumanne Fadhil, Lambert Sadianka, Freddy
Chudu/Juma Seif dk48, Mohammed Mkopi, Jeremiah Juma na Leonce Mutalemwa/Meshack
Suleiman dk51.
MATOKEO YOTE KWA UJUMLA
FT
|
T.PRISONS
|
2
|
:
|
2
|
YANGA
|
FT
|
SIMBA SC
|
5
|
:
|
1
|
MGAMBO JKT
|
FT
|
KAGERA SUGAR
|
2
|
:
|
1
|
MAJIMAJI
|
JKT RUVU
|
0
|
:
|
0
|
MBEYA CITY
|
|
FT
|
AFRICAN SPORT
|
1
|
:
|
0
|
MWADUI FC
|
FT
|
MTIBWA SUGAR
|
2
|
:
|
2
|
TOTO AFRICANS
|
Orodha ya Wafungaji Bora Ligi Kuu Msimu Huu
Rn | Player Name | Timu | Goal |
---|---|---|---|
1 | Amisi Tambwe | Yanga SC | 14 |
2 | Hamisi Kiiza | Simba SC | 14 |
3 | Jerema Juma | T.Prisons | 10 |
4 | Donald Ngoma | Yanga SC | 9 |
5 | Elias Maguli | Stand United | 9 |
6 | Ibrahim Ajibu | Simba SC | 7 |
7 | Kipre Tcheche | Azam FC | 7 |
8 | Shomari Kapombe | Azam FC | 7 |
9 | Atupele Green | Ndanda FC | 6 |
10 | John Bocco | Azam FC | 6 |
11 | Fully Zully Maganga | Mgambo JKT | 5 |
12 | Mohammed Mkopi | T.Prisons | 5 |
13 | Paul Nonga | Mwadui FC | 5 |
14 | Thaban Kamusoko | Yanga SC | 5 |
15 | Didier Kavumbagu | Azam FC | 4 |
16 | Edward Christopher | Toto Africans | 4 |
17 | Jery Tegete | Mwadui FC | 4 |
18 | Miraji Athuman | Toto Africans | 4 |
19 | Omary Mponda | Ndanda FC | 4 |
20 | Saimon Msuva | Yanga SC | 4 |
Msimamo wa Ligi Kuu Msimu Huu
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | YANGA | 17 | 12 | 4 | 1 | 38 | 9 | 29 | 40 |
2 | SIMBA SC | 17 | 12 | 3 | 2 | 32 | 10 | 22 | 39 |
3 | Azam FC | 15 | 12 | 3 | 0 | 30 | 10 | 20 | 39 |
4 | MTIBWA SUGAR | 17 | 9 | 5 | 3 | 20 | 11 | 9 | 32 |
5 | MWADUI FC | 17 | 8 | 4 | 5 | 19 | 15 | 4 | 28 |
6 | STAND UNITED | 16 | 9 | 1 | 6 | 17 | 13 | 4 | 28 |
7 | T. PRISONS | 16 | 8 | 4 | 4 | 18 | 17 | 1 | 28 |
8 | TOTO AFRICANS | 17 | 4 | 6 | 7 | 15 | 21 | -6 | 18 |
9 | MGAMBO SHOOTING | 16 | 4 | 5 | 7 | 14 | 17 | -3 | 17 |
10 | KAGERA SUGAR | 17 | 4 | 3 | 10 | 9 | 20 | -11 | 15 |
11 | MBEYA CITY | 16 | 3 | 5 | 8 | 13 | 21 | -8 | 14 |
12 | NDANDA FC | 16 | 2 | 7 | 7 | 14 | 18 | -4 | 13 |
13 | Coastal Union | 16 | 2 | 7 | 7 | 11 | 17 | -6 | 13 |
14 | JKT RUVU | 16 | 3 | 4 | 9 | 16 | 23 | -7 | 13 |
15 | MAJIMAJI FC | 17 | 3 | 4 | 10 | 10 | 31 | -21 | 13 |
16 | AFRICAN SPORT | 17 | 3 | 3 | 11 | 5 | 19 | -14 | 12 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni