Chelsea wameendeleza rekodi yao ya
kutoshindwa chini ya kaimu meneja Guus Hiddink hadi mechi saba katika
Ligi ya Premia baada ya kutoka sare tasa na Watford.
Heurelho Gomes alifanya kazi ya ziada kuzima mpira wa kichwa kutoka kwa Costa akitumia mkono mmoja na kuwanyima Chelsea ushindi dakika za mwisho mwisho.
Chelsea wamepanda alama moja hadi nambari 13 na alama 29, huku Watford wakiwa alama nne na nafasi nne juu ya Chelsea.
Kwingineko, Everton walipata ushindi wao wa kwanza ligini nyumbani tangu Novemba walipoandikisha ushindi dhidi ya Newcastle uwanjani Goodison Park.
Everton, ambao hawakuwa wameshinda mechi hata moja Ligi ya Premia tangu siku ya Boxing Day, walijiweka kifua mbele kupitia Aaron Lennon.
Ross Barkley Barkley baadaye alifunga mikwaju miwili ya penalti, ya pili ikitokana na madhambi ya Jamaal Lascelles ambaye alilishwa kadi nyekundu.
Vijana hao wa Roberto Martinez sasa wamepanda hadi nambari 11 ligini, huku Newcastle nao wakisalia nambari 18, alama mbili kutoka eneo la kushushwa daraja.
Kule nchini Hispania Barcelona imeifunga timu ya Valencia ya Garry Neville magoli 7-0
Messi alifunga magoli matatu wakati mchezaji aliye kwenye kiwango cha hali juu Luis Suarez akifunga magoli manne wakati Neymar akikosa mkwaju wa penati kwenye mchezo huo
Wednesday, February 3, 2016
Premier League | ||||
---|---|---|---|---|
FT |
Everton
|
3 - 0
|
Newcastle United
|
|
FT |
Watford
|
0 - 0
|
Chelsea
|
Serie A | ||||
---|---|---|---|---|
FT |
Empoli
|
1 - 1
|
Udinese
|
|
FT |
Fiorentina
|
2 - 1
|
Carpi
|
|
FT |
Frosinone
|
1 - 0
|
Bologna
|
|
FT |
Hellas Verona
|
2 - 1
|
Atalanta
|
|
FT |
Internazionale
|
1 - 0
|
Chievo
|
|
FT |
Juventus
|
1 - 0
|
Genoa
|
|
FT |
Lazio
|
0 - 2
|
Napoli
|
|
FT |
Palermo
|
0 - 2
|
Milan
|
|
FT |
Sampdoria
|
2 - 2
|
Torino
|
Ligue 1 | ||||
---|---|---|---|---|
FT |
Guingamp
|
4 - 0
|
Troyes
|
|
FT |
Lille
|
1 - 0
|
Caen
|
|
FT |
Nantes
|
3 - 1
|
Gazélec Ajaccio
|
|
FT |
Nice
|
1 - 0
|
Toulouse
|
|
FT |
Olympique Lyonnais
|
3 - 0
|
Bordeaux
|
|
FT |
PSG
|
3 - 1
|
Lorient
|
|
FT |
Reims
|
2 - 1
|
Angers
|
Copa del Rey |
||||
---|---|---|---|---|
FT |
Barcelona
|
7 - 0
|
Valencia
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni