
Yanga itaondoka Dar kuelekea Mauritius ikiwa na kikosi cha wachezaji 21, viongozi wa 7 wa benchi la ufundi pamoja na mkuu wa msafara Ayoub Nyenzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.
Wachezaji ambao hawato safari na timu ni Geofrey Mwashiuya, Benedict Tinoco ambao wanashughulikia passport zao za kusafiria pamoja na Matteo Anthony ambaye hayuko fiti kimchezo.
Mchezo wa Yanga dhidi ya Cercle De Joachim umepangwa kuchezwa siku ya Jumamosi February 13 saa 9:30 alasiri kwa saa za Mauritius na utasimamiwa na waamuzi kutoka Madagascar wakati match commissioner anatoka Msumbiji.
Kwa mujibu wa afisa habari wa Yanga Jerry Muro, mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Yanga hakita rejea moja kwa moja nchini bali kitaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuhezwa February 20 mwaka huu.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni