.

PSG imetinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga timu hiyo kwenye michezo yote, nyumbani na ugenini, hivyo Chelsea kuenguliwa kwa jumla ya mabao 4-2.
Mabao ya PSG yamewekwa kambani na nyota wake Zlatan Ibrahimovic na Rabiot huku lile la kufutia machozi kwa upande wa Chelsea likiwekwa kambani na mshambuliaji wake Diego Costa.
Kwa ushindi huo Chelsea inaungana na timu za Zenit Saint Petersburg iliyosukumizwa nje ya mashindano na Benfica kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa pili huku jumla ikiwa ni mabao 3-1.
AS Roma na Gent zilizotangulia kutoka hapo Jana.
Timu zilizofuzu kutinga hatua ya robo fainali ni Real Madrid, Wolfsburg, Benfica na PSG.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni