Liverpool wameanza vyema kampeni zao kwenye michuano ya Europa League hatua ya 16 bora baada ya kuiangushia kipigo Manchester United cha bao 2-0 kwenye uwanja wa Anfeild jana usiku.
Kikosi cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa ya mchezo huo wa kwanza kati ya timu hizo za Premier League giants huku kocha huyo wa kijerumani akifurahia ushindi wake dhidi ya United.
Daniel Sturridge aliipa Liverpool goli la kuongoza dakika ya 15 kwa mkwaju wa penati baada ya Memphis Depay kumfanyia madhambi Nathaniel Clyne kwenye eneo la hatari penati ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wadau wakikosoa kwamba ilikuwa ni nje ya penalty box.
Roberto Firmino akaongeza bao jingine kwa shuti kali la karibu zikiwa zimesalia dakika 17 pekee mchezo huo kumalizika.
United haikutengeneza hata nafasi moja ya kufunga, ubora wa golikipa wao David de Gea ndiyo umeikoa United kuchezea idadi kubwa ya magoli kwenye mchezo huo baada ya mlinda mlango huyo wa Hispania kuokoa michomo mingi.
Rekodi zilizowekwa kwenye mchezo huo:
- Manchester United hawajashinda mchezo wowote wa ugenini kati ya michezo yao sita iliyopita kwenye hatua ya moano ya michuano ya Ulaya, wamepoteza michezo mitano kati ya hiyo.
- United imepata clean sheet moja kwenye mechi 10 walizocheza kwenye uwanja wa Anfield kwenye mechi za mashindano yote.
- Daniel Sturridge amefunga magoli matano na ku-assist goli moja kwenye mechi saba dhidi ya United kwenye mashindano yote.
- United wamepigiwa mashuti nane on target dhidi ya Liverpool, mashuti mengi zaidi kuziuwa na klabu hiyo ndani ya mechi moja msimu huu.
- Roberto Firmino amefunga magoli matatu mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye mechi za Liverpool.
Mchezo
mwingine, Borussia Dortmund imeanza vyema kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya
Tottenham Hotspur ya England mabao ya Pierre-Emerick Aubameyang dakika
ya 30 na Marco Reus dakika ya 61 na 70 Uwanja wa Signal Iduna Park mjini
Dortmund, Ujerumani.
Sparta
Prague imelazimishwa sare ya 1-1 na Lazio Uwanja wa Jenerali, bao lao
likifungwa na Martin Frydek dakika ya 13, kabla ya Marco Parolo
kuwasawazishia wageni dakika ya 38, wakati Athletic Club imeshinda 1-0
dhidi ya Valencia CF, bao pekee la Raul Garcia Escudero dakika ya 20
Uwanja wa San Mames.
Villarreal
imeshinda 2-0 dhidi ya Bayer 04 Leverkusen, mabao ya Cedric Bakambu
dakika ya nne na 56 Uwanja wa El Madrigal, wakati FC Basel imetoka sare
ya 0-0 na Sevilla Uwanja wa St Jakob-Park.
Fenerbahce
imeshinda 1-0 dhidi ya Sporting Braga, bao pekee la Mehmet Topal dakika
ya 82 Uwanja wa Ulker Stadyumu, wakati Shakhtar Donetsk imeichapa 3-1
RSC Anderlecht, mabao yake yakifungwa na Taison Barcellos Freda dakika
ya 21, Olexandr Kucher dakika ya 24 na Eduardo Alves da Silva dakika ya
79, huku la wageni likifungwa na Frank Acheampong dakika ya 68 Uwanja wa
Lviv.
Mechi zote za marudiano zitafanyika Machi 17 na washindi wa jumla watakwenda Robo Fainali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni