
Nyota namba moja wa zamani wa mchezo
wa Tenesi Maria Sharapova amethibitisha kushindwa vipimo baada ya
kubainika alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika michuano
ya wazi ya Australia Mwaka huu.



Katika siku chache zilizopita nimepata barua kutoka ITF (shirikisho la tenesi la kimataifa) na nikagundua kuwa dawa hizo zina jina jingine la meldonium,
"Ni muhimu sana kuelewa kwa miaka 10 dawa hizi hazikua kwenye orodha ya shirika la kudhibiti matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni (Wada).

"Lakini sheria zilibadilika mwezi January na kuzifanya dawa za meldonium kukatazwa, kitu ambacho sikufahamu, mwezi Desemba tarehe 22 nilipata barua pepe toka Wada kuhusu mabadiliko kwa dawa zilizokatazwa, ila sikufungua hiyo linki''.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni