STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 2 Machi 2016

LIGI KUU BARA,TANGA KUNANI?



 
LIGI Kuu Bara imebakisha takribani mechi kumi kumalizika kwa msimu wa 2015/16 ambapo mpaka sasa Yanga ndiyo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 46.

Mwishoni mwa msimu huu timu tatu zinatarajiwa kushuka daraja baada ya mbili kutoka Ligi Daraja la Kwanza kupanda huku moja kutoka Kundi C ikisubiri uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Kutokana na mwenendo wa ligi ulivyo kwa sasa, kuna hatari msimu ujao tukazikosa timu mbili au hata zote tatu kutoka mkoani Tanga kama hawatashtukia mchezo mapema.

Timu za mkoa huo zimekuwa hazifanyi vizuri msimu huu, mpaka sasa zote zipo kwenye hatari ya kushuka daraja na lolote linaweza kutokea mwishoni mwa msimu hapo Mei 7 ambapo mechi za mwisho zitapigwa.

Mgambo JKT, African Sports na Coastal Union, ndizo timu tatu kutoka Tanga zinazouwakilisha mkoa huo ambao kwa muda mrefu umekuwa na timu ya ligi kuu tofauti na mikoa mingine.

Katika msimamo wa ligi mpaka sasa, Mgambo inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 18, Coastal ya 14 ikiwa na pointi 16 huku African Sports ikishika nafasi ya 15, pointi 16. Utaona hapo timu hizo zote hazijapishana sana kwa pointi hali ambayo inaonyesha wazi kuwa wote wapo kwenye hatari.

Zote zinatumia Uwanja wa Mkwakwani kwa mechi zao za nyumbani na kwenye mechi hizo zilizobaki, Coastal itacheza hapo mechi tano, Mgambo sita na African Sports saba


                                  
                                  MECHI ZILIZO HATARI KWAO:

Ukiangalia ratiba ya ligi, timu hizo zote zimebakisha mechi kumi na kwenye mechi hizo zote zimebakiwa na michezo minne ambayo unaweza kusema ni migumu na umakini na upambanaji wa kweli unahitaji ili kupata pointi ambazo zitawaweka sehemu salama.

Zote zitacheza dhidi ya JKT Ruvu ambayo inahaha isishuke daraja kutokana na sasa kuwa mkiani, utaona hapo ni kwa kiasi gani mechi hizo zitakuwa ngumu kiasi gani.

African Sports ndiyo itaanza kucheza na JKT Ruvu, mchezo wao utapigwa Aprili 3 kwenye Uwanja wa Karume, Dar. Kisha Coastal itacheza na timu hiyo siku saba mbele katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, huku siku ya mwisho ya kuhitimisha msimu huu, Mgambo itapambana na Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani.

Mbali na mechi dhidi ya Ruvu, timu hizo pia zitapambana zenyewe. Machi 9, Mgambo itakuwa mwenyeji wa Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani, kisha Aprili 16, African Sports itapambana na Coastal kwenye uwanja huohuo.



Wanakutana na wanaosaka ubingwa

Timu za Yanga, Azam na Simba, zote zipo kwenye harakati za kuwania ubingwa wa ligi kutokana na kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi, Yanga ina pointi 46, Azam (46) na Simba (45), huku inayofuata baada ya hizo ni Mtibwa yenye pointi 33.

Katika mechi kumi zilizobaki kwa timu hizo za Tanga, Coastal kidogo imepata ahueni kutokana na kuwa na mchezo mmoja tu dhidi ya Simba, lakini African Sports na Mgambo zitakutana na Yanga pia na Azam. Yaani kila moja itacheza mechi mbili na Yanga na Azam.


http://simbasports.co.tz/file/2015/09/african-sports.png

                               MECHI ZA AFRICAN SPORTS:

Sports Vs Majimaji-Mkwakwani

Yanga Vs Sports-Taifa

Sports Vs Mbeya-Mkwakwani

Sports Vs Prisons-Mkwakwani

JKT Ruvu Vs Sports-Karume

Sports Vs Kagera-Mkwakwani

Sports Vs Coastal-Mkwakwani

Sports Vs Toto-Mkwakwani

Sports Vs Azam-Mkwakwani

Mtibwa Vs Sports-Manungu


 
https://img.sportdata.co/football/image/11785b

                            MECHI ZA MGAMBO ZILIZOBAKI:


Kagera Vs Mgambo-Kambarage

Coastal Vs Mgambo-Mkwakwani

Mgambo Vs Mwadui-Mkwakwani

Mgambo Vs Toto-Mkwakwani

Stand Vs Mgambo-Kambarage

Mgambo Vs Mbeya City-Mkwakwani

Yanga Vs Mgambo-Taifa

Mgambo Vs Mtibwa-Mkwakwani

Mgambo Vs JKT Ruvu-Mkwakwani

Azam Vs Mgambo-Azam Complex





                                 
                              MECHI ZA COASTAL ZILIZOBAKI:

Mtibwa Vs Coastal-Manungu

Coastal Vs Mgambo-Mkwakwani

Kagera Vs Coastal-Kambarage

Coastal Vs Simba-Mkwakwani

Mbeya Vs Coastal-Sokoine

Coastal Vs JKT Ruvu-Mkwakwani

Sports Vs Coastal-Mkwakwani

Stand Vs Coastal-Kambarage

Majimaji Vs Coastal-Majimaji

Coastal Vs Prisons-Mkwakwani



 www.mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox