
Kwa wapenzi wa michezo ya game hususani game za mchezo wa soka maarufu kama Play Station,
huwa ni kawaida kuona wataalam wa game kutengeneza game za timu
zinazopendwa na muonekano wa wachezaji wa timu husika lengo likiwa
kujenga taswira halisi kwa mchezaji wa game.

muonekano wa Lionel Messi katika Game ya FIFA 16.
Mbwana Samatta ambaye amejiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kongo kwa dau linalotajwa kuwa ni euro 800,000, ameingizwa katika ya Play Station ya FIFA 16.

Huu ndio muonekano wa Mbwana Samatta ambapo kwa taarifa zisizo rasmi anatajwa kuwa huenda akawa mtanzania wa kwanza kuwemo katika Game ya FIFA 16.
Samatta
yupo katika game hiyo na nimekutana na muonekano wake sambamba na namba
yake ya jezi 77 anayotumia, kwa ripoti zisizo rasmi huenda Mbwana Samatta ndio akawa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuwemo katika hiyo.

Muonekano wa wachezaji wa FC Barcelona akiwemo Neymar wa kwanza kulia katika Game ya FIFA 16
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni