Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
ana wasiwasi kuhusu matokeo ya timu yake na anasema wachezaji wake
wanafaa kuimarika baada ya kushindwa 2-1 na kilabu ya Swansea.
Mauricio Pochettino,wakati huohuo amekataa kulaumu mtu baada ya timu yake ya Tottenham Hotspur inayopigania kuchukua ligi msimu huu kupoteza kwa West Ham 1-0.
Na mkufunzi wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema kuwa hafikirii kushinda taji la ligi ya Uingereza baada ya timu yake kucharazwa 3-0 na Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Hiyo inamaanisha kwamba Leicester itasalia kileleni mwa ligi huku ikiwa kumesalia mechi 10 pekee.
Leicester ina pointi 57, na hivyobasi wameongeza uongozi wao katika jedwali la ligi hiyo baada ya sare ya 2-2 dhidi ya West Bromwich.
Ushindi huo wa Swansea unamaanisha kwamba Arsenal imepoteza mara tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.
WAKATU HUOHUO Arsenal watamkosa mlinda lango wao
Petr Cech mechi kali dhidi ya mahasimu wao wa London Tottenham Hotspur
uwanjani White Hart Lane Jumamosi.
Cech aliumia dakika za mwishomwisho za mechi ambayo walilazwa 2-1 nyumbani na Swansea City baada yake kuruka juu kufikia mpira wakati wa kona.
"Alikuwa anatatizwa kiasi na mtoki kabla ya mechi na nadhani amesumbuka kwenye mechi hii,” meneja wao Arsene Wenger alisema baada ya mechi hiyo.
Beki wao Laurent Koscielny pia hataweza kuwachezea debi hiyo ya London kutokana na jeraha mguuni.
Koscielny, 30, hakuwachezea mechi dhidi ya Swansea.
Cech, 33, aliyehamia Emirates kutoka Chelsea, amewachezea Gunners mechi 28 Ligi ya Premia.
Arsenal wataenda kwenye mechi hiyo wakiwa nafasi ya tatu kwenye jedwali, alama sita nyuma ya viongozi Leicester City, zikiwa zimesalia mechi 10 msimu huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni