MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC iliyokuwa ifanyike Jumatano Saa 10:30 jioni Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro imefutwa na sasa itapangiwa siku nyingine.
Kufutwa kwa mechi hiyo kumetokana na Azam FC kusafiri keshokutwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits ya huko.
Michezo saba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuchezwa katikati ya wiki hii, kwa kesho kuchezwa mchezo mmoja, huku michezo mingine sita ikichezwa siku za Jumatano na Alhamisi katika viwanja mbalimbali nchini.
Kesho Jumanne, Young Africans watakua wenyeji wa Wana Kimanumanu African Sports, mchezo utakaoanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Jumatano Machi 09, 2016 Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Coastal Union wakicheza na ndugu zao maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mwadui FC watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Toto African katika uwanja wa Mabatini , Mlandizi mkoa wa Pwani.
Alhamisi Simba SC watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya timu ya Mbeya City wakiwakaribisha Stand United chama la wana katika uwanja wa Sokoine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni