Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Charles Boniface
Mkwasa kesho anatarajiwa kutangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili
za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Chad.
Mkwasa anatarajiwa kutangaza kikosi ambacho hakitarajiwi kuwa na
mabadiliko makubwa sana kutokana na viwango vya wachezaji waliopo Taifa
Stars na wale ambao wanaopigania kuitwa.
Swali kubwa ni pengo la Nadir Haroub ambaye alikuwa akiunda safu ya ulinzi pamoja na pacha wake wa klabuni, Kelvin Yondani.
Beki huyo mkongwe ambaye ameitumikia Taifa Stars kwa miaka kadhaa
alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa kufuatia kuvuliwa unahodha
na jukumu hilo kukabidhiwa kwa Mbwana Samatta.
Aggrey Morris alitarajiwa kuwa mbadala wa Cannavaro lakini amekuwa
nje kwa muda mrefu kwenye klabu yake ya Azam kutokana kuwa na majeruhi
hivyo kushindwa kuthibitisha makali yake mbele ya macho ya Mkwasa ambaye
huenda angemzingatia kwa kumjumuisha kikosini.
David Mwantika wa Azam ambaye amekuwa akicheza na Pascal wawa anaweza
kutupiwa jicho na Mkwasa kama ilivyo kwa Erasto Nyoni ambaye anamudu
kucheza katikati na pembeni.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 7 Machi 2016
MKWASA KUTANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS KESHO,
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni