STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 7 Mei 2016

COASTAL UNION RASMI YASHUKA DARAJA, MATOKEO YOTE YAPO HAPA, ANGALIA MSIMAMO ULIVYO



Rasmi Coastal union yashuka daraja hii leo baada ya kufungwa goli 2-1 na Stand united katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Katika mchezo wa leo Coastal union iliingia uwanjani bila ya nyota wake 7 ambao waligoma kuongozana na timu hiyo mkoani Shinyanga.

Katika mchezo huo Stand united walianza kwa kasi huku Coastal union wakianza kwa kujiami na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza na kutengewnza nafasi kadhaa walizo shindwa kuzitumia.

Katika dakika ya 29 Stand united walipata penati ambayo Elius Maguli aliiandikia goli la kuongoza Stand kwa mkwaju huo wa penati.
Kuingia kwa goli hilo kuliongeza kasi ya mchezo huku timu zote mbilia zikiendelea kupoteza nafasi za kufunga magoli na kupeleka dakika 45 za kwanza kumalizika kwa Stand united kuwambele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili Coastal union walirejea kwa kucheza mipira mirefu, huku Stand united wakijaribu kutawala mchezo, na katika dakika ya 46 Elius Maguli aliianikia Stand united goli la 2.

Coastal union walireja mchezoni katika dakika ya 64 baada ya Said Jeilani kuindika Coastal union goli la kufutia machozi na kupeleka mchezo kumalizika kwa Coastal union kufungwa goli 2-1.

Kwa matokeo hayo Coastal union wameshuka daraja rasmi, na msimu ujao hawatokuwepo katika ligi kuu ya vodacom.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Mabatini, JKT Ruvu wameendelea kulikwepa janga la kushuka daraja baada ya leo kuifunga goli 2-0 Ndanda FC.

MATOKEO LIGI KUU LEO
MGAMBO JKT 1-1 MTIBWA SUGAR
STAND UNITED 2-1 COASTAL UNION
JKT RUVU 2-0 NDANDA FC

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM
Rn
Timu
P
W
D
L
F
A
Gd
Pts
1
YANGA
27
21
5
1
64
16
48
68
2
SIMBA SC
26
18
4
4
43
14
29
58
3
Azam FC
27
16
9
2
42
21
21
57
4
MTIBWA SUGAR
28
13
8
7
31
20
11
47
5
T. PRISONS
27
10
12
5
24
22
2
42
6
MWADUI FC
27
10
7
10
27
26
1
37
7
STAND UNITED
28
11
4
13
26
28
-2
37
8
MBEYA CITY
27
9
6
12
31
31
0
33
9
NDANDA FC
28
7
12
9
26
29
-3
33
10
MAJIMAJI FC
27
9
6
12
20
36
-16
33
11
TOTO AFRICANS
28
7
9
12
26
38
-12
30
12
JKT RUVU
28
7
8
13
29
37
-8
29
13
AFRICAN SPORT
28
7
5
16
12
30
-18
26
14
KAGERA SUGAR
27
6
7
14
19
31
-12
25
15
MGAMBO SHOOTING
28
5
9
14
22
35
-13
24
16
Coastal Union
29
5
7
17
17
40
-23
22

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox