Manchester United wametoka nyuma na kuichapa Crystal Palace na kutwaa kombe la FA Cup kwenye uwanja wa Wembley kupitia goli la ushindi la Jesse Lingard katika muda wa nyongeza baada ya sare ya goli 1-1 kwenye dakika 90.
Huku kukiwa na tetesi kwamba mchezo huo huenda ukawa wa mwisho kwa kocha Louis van Gaal kama manager wa Manchester United, lakini ameweza kuongeza taji maarufu kwenye maisha yake ya soka akiwa England.
United wangelikosa taji hilo inamaanisha walikuwa wanamaliza msimu huu bila taji lolote huku wakiwa wameshapoteza nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya, Jason Puncheon aliongeza maumivu kwa United baada ya kukandamiza bao lililoiweka mbele Palace zikiwa zimesalia dakika 12 pambano kumalizika.
Goli la Puncheon lilikuwa ni mwiba kwa United lakini wakali hao wa Old Trafford walisawazisha bao hilo dakika nne baadaye kwa Mata kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Wayne Rooney.
Beki wa Manchester United Chris Smalling alioneshwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Yannick Bolasie wakati wa muda wa nyongeza lakini Lingard akapeleka shangwe Old Trafford kwa kufunga bao la ushindi na kuipa United taji la FA.
PICHA KOCHA WA C.PALACE,ALAN PARDEW AKICHEZA BAADA YA PUNCHEON ALIPOFUNGA GOLI;
- Manchester United sasa wametwaa FA Cup kwa mara ya 12 na kuifikia rekodi ya Arsenal
- Louis van Gaal ni kocha wa tatu kutoka Uholanzi kufanikiwa kushinda FA Cup, akitanguliwa na Guus Hiddink na Ruud Gullit.
- Goli la ushindi la Jesse Lingard lilikuwa la kwanza kwenye michezo 18 aliyocheza kwenye mashindano yote.
- Chris Smalling ni mchezaji wanne lakini ni wa kwanza kutoka England kupewa kadi nyekundu kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup wengine waliowahi kupewa kadi nyekundu kwenye fainali ya FA Cup ni (Kevin Moran 1985, Jose Reyes 2005 and Pablo Zabaleta 2013).
- Manchester United wameshinda michezo yote ya fainali za FA Cup iliyohusisha wachezaji wake kutolewa kwa kadi nyekundu (1985 and 2016).
FAINALI YA DFP-POKAL
Bayern Munich imeishinda Borussia Dortmund kwa penalti 4-3 na kubeba ubingwa wa Kombe la Ujerumani.
Huo ni ushindi wa 11 kwa Bayern kushinda makombe mawili ya Bundesliga na Kombe la Ujerumani kwa wakati mmoja.
Lakini
klabu hiyo, imemuaga vizuri kocha Pep Guardiola ambaye alishindwa
kujizuia na kumwaga chozi. Kocha huyo anaondoka na kwenda kujiunga na
Manchester City.
Timu hizo zilicheza kwa dakika 120 bila kupata mshindi na zikalazimika kupigiana mikwaju ya penalti.
Kipa nyota wa Bayern, Manuel Neuer aliokoa mkwaju ya Sven Bender na Sokratis Papastathopoulos akakosa.
Kipa
mzoefu wa Dortmund, Roman Buerki aliokoa mkwaju wa Joshua Kimmich
lakini Thomas Muller akafunga na kuifanya Bayern iendelee kubaki kwenye
msitari.
COUPE DE FRANCE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni