Hatimaye tetesi zinageuka kuwa kweli, Manchester United watamtangaza
Jose Mourinho kuwa kocha wao, shirika la utangazaji la Uingereza BBC
limeripoti.
Mourinho amekuwa nje ya kazi tangu alipofukuzwa kazi na Chelsea mnamo December 2015.
Huku United wakiwa wameshindwa kufuzu kucheza Champions League chini
ya Louis van Gaal – viongozi wa Old Trafford wameamua kufanya
mabadiliko.
Inaeleweka dili na kocha huyo mwenye miaka 53 lilifanyika kabla ya mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace.
United wanategemewa kumtangaza rasmi Mourinho mapema wiki ijayo baada ya kumtaarifu Van Gaal kuhusu mwisho wa ajira yake.
Van Gaal bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa miaka 3, lakini
pamoja na kutumia £250m utawala wake umekuwa wa majuto kwa klabu na
kuwaacha mashabiki wengi wakiwa hawaridhiki na utendaji wake, msimu wa
kwanza alimaliza nafasi ya 4, na msimu huu watano.
Mourinho ni mmoja wa makocha bora katika ulimwengu wa soka, akishinda
makombe matatu ya ligi katika vipindi viwili vya kazi ndani ya Chelsea,
pamoja kuziongoza Porto na Inter Milan kutwaa Champions League – pia
akibeba ubingwa wa La Liga na RealMadrid.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumapili, 22 Mei 2016
JOSE MOURINHO KASHATUA MANCHESTER UNITED.............
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni