STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 12 Mei 2016

LISTI YA VILABU TAJIRI NA WACHEZAJI WALIOVUTA MKWANJA MREFU 2015...........

 



Mapato makubwa ya fedha zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya TV , mauzo jezi na mapato ya udhamini wa jezi, wadhamini na ushiriki wa Champions league umeendelea kuzipa uthamani mkubwa vilabu vya soka duniani. 

  Matokeo yake, wawekezaji ambao waliwekeza kwenye soka katika kipindi cha mika 10 iliyopita sasa wanavuna mapato makubwa hasa katika timu za England. 

UEFA imeongeza malipo katika Champions League kwa asilimia 50% kwa miaka 3 kuanzia msimu wa 2015-16. 

Fainali ya mwaka huu, itakayochezwa San Siro jijini Milan, Italy, baina ya vilabu vya Spain, Real Madrid vs Atletico, kila timu itapata kiasi cha $100 million.

Mapato ya Champions League msimu uliopita

Vilabu 20 ambavyo vinaongoza kwa uthamani vina thamani ya wastani wa $1.44 billion, ongezeko la 24% kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.



 Malipo makubwa ya dili za TV, kama mkataba wa miaka  3 wenye thamani ya $7.9 billion baina ya English Premier League na Sky Sports na BTSport ambao unaanza msimu wa 2016/17, na dili nyingine za udhamini wa jezi, mfano ukiwa mkataba wenye thamani ya $130m kwa mwaka baina ya Manchester United na Adidas. 
 
 

Timu yenye thamani kubwa ya soka kwa mwaka wa nne mfululizo ni Real Madrid wakiwa na thamani ya $3.65 billion, ongezeko la 12% la thamani waliyokuwa nayo mwaka uliopita. 


 Wanaowafuatia ni FC Barcelona ambao wana thamani ya $3.55 billion, ongezeko la 12% la thamani kutoka msimu uliopita.  

 
Barcelona huenda wakawapita wapinzani wao kutokana na mkataba wa $400 million la utengenezaji upya uwanja wao wa Camp Nou, ambao unategemea kukamilika ndani ya miaka mitano. 

  

Timu ya 3 kwa thamani kubwa ni Manchester United, klabu ambayo ipo kwenye soko la hisa. 

Forbes wanaitaja kuwa na thamani ya $3.32billion, ongezeko la asilimia 7 la thamani kutoka mwaka jana. Man United wametengeneza faida ya $190m kwa msimu wa 2014-15, kwenye listi  hii Man United ndio timu iliyoingiza faida kubwa kwa upande wa soka lakini wapo nyuma ya  Dallas Cowboys ($270 million) na New England Patriots ($195 million) kiujumla.


Wakati Real Madrid wakitajwa kuwa kuwa klabu ya soka yenye thamani zaidi duniani, huku Manchester United wakitajwa kuwa klabu iliyotengeneza faida kubwa zaidi kwa mwaka uliopita, pia imetolewa listi ya wachezaji waliotengeneza fedha nyingi zaidi mwaka jana.

image

Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mwanasoka aliyetengeneza fedha nyingi duniani na pia mwanamichezo ambaye bado anacheza ambaye analipwa fedha nyingi zaidi – kwa mujibu wa jarida la masuala ya fedha la kimarekani Forbes.

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ameripotiwa kuwa alilipwa kiasi cha $82 million (£56.7m), huku mapato ya mshahara ni kiasi cha $53m (£36.7m) na $29m (£20m) ikitokana na matangazo ya biashara.

image

Nahodha huyo wa Ureno, ambaye aliweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi wakati aliposajiliwa kutoka Manchester United kwenda Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 80 mnamo mwaka 2009, alisaini mkataba mpya na Real Madrid mwaka 2013.

Forbes, imemtangaza Ronaldo kuwa mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi kuliko yoyote duniani kwa sasa.

image

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, mshindi wa tuzo ya  2015 FIFA Ballon d’Or, ameshika nafasi ya pili akitengeneza kiasi cha  $77m (£53.3m), kiasi cha $51m (£35.3m) kikitokana na mshahara na kiasi cha $26m (£18m) kikitokana na matangazo ya biashara.  

Nahodha huyu wa Argentina alisaini mkataba mpya na Barca mwaka 2014.

Forbes imeripoti kwamba  Ronaldo ametengeneza kiasi cha $550m (£380.9m) katika kipinfi cha miaka yake 14 ya kucheza soka la ushindani, kuanzia Sporting Lisbob, wakati Messi ambahe maisha yake yote ameitumikia Barcelona ametengeneza kiasi cha $450m (£311.5m) ndani ya miaka 11.

image

Mcheza basketball Kobe Bryant, ambaye alistaafu mwishoni mwa mwezi uliopita, ndio mwanamichezo pekee ambaye ametengeneza fedha nyingi kuliko Ronaldo kwa ujumla – akitengeneza kiasi cha $680m (£470.8m) katika miaka 17 ya kucheza NBA.

Ronaldo na  Messi, ambao wamekuwa washindi wa tuzo ya Ballon D’or tangu Ricardo Kaka aliposhinda tuzo hiyo mwaka 2007,  wamemuacha mbali anayeshika nafasi ya 3, Zlatan Ibrahimovic.

image

Nahodha wa Sweden, mwenye umri wa miaka 34, ameingiza kiasi cha $37m (£25.6m) kupitia mshahara wake na PSG, huku $7m (£4.84m) zikitokana na mikataba wa biashara.

Mshambuliaji wa kibrazil Neymar ameshika nafasi ya 4, akiingiza kiasi cha $36m sawa na £24.9.

image

Forbes wameripoti kwamba Neymar ndio mchezaji ambaye ametengeneza fedha nyingi zaidi kupitia matangazo ya biashara – kiasi cha $22million kuliko mapato ya mshahara wake $14millioni.

LISTI YA WACHEZAJI WALIOTENGENEZA FEDHA NYINGI 2015:

image

1 Cristiano Ronaldo (Real Madrid): $82m (£56.7m)

2 Lionel Messi (Barcelona): $77m (£53.3m)


3 Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain): $37m (£25.6m)


4 Neymar (Barcelona): $36m (£24.9m)


5 Gareth Bale (Real Madrid): $34m (£23.5m)

6. Wayne Rooney (Manchester United) | $26m

7. Sergio Aguero | $24m

8 Luis Suarez (Barcelona) | $23m

9. Eden Hazard (Chelsea) | $22m

10. Cesc Fabregas (Chelsea) | $21m

11. James Rodriguez (Real Madrid) | $21m

12. Yaya Toure (Manchester City) | $20m

13. Radamel Falcao (Chelsea) | $19m

14. Thiago Silva (Paris Saint-Germain) | $18m

15. Mesut Ozil (Arsenal) | $18m

16. Bastian Schweinsteiger (Manchester United) | $18m

17. Angel Di Maria (Paris Saint-Germain) | $18m

18. Robin van Persie (Fenerbahce) | $17m

19. David Silva (Manchester City) | $17m

20. Samir Nasri (Manchester City) | $15m




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox