Klabu ya West Ham United iliaga
uwanja wake wa nyumbani wa Upton Park kwa kuvuruga juhudi za Manchester
United za kutaka kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne.

Kwenye mechi hiyo ya kusisimua, West Ham walichomoza na ushindi wa 3-2.


West Ham walitangulia kupitia bao la Diafra Sakho kipindi cha kwanza, lakini Antony Martial aliwasawazishia Red Devils kwa bao dakika ya 51 na kisha akawaweka kifua mbele dakika ya 72.
West Ham, hata hivyo, walijikwamua kwa kufunga mabao mawili ya kichwa katika kipindi cha dakika nne kupitia Michail Antonio na Winston Reid aliefunga goli la mwisho katika uwanja huo ikiwa ni kumbukumbu kubwa katika historia yake na klabu kwa ujumla.

Wamo alama moja nyuma ya Manchester United na watazuru Stoke Jumapili.
Manchester United, watakuwa wenyeji wa Bournemouth, mechi ambayo watahitajika kushinda kujiimarishia uwezekano wa kumaliza katika nne bora.

Mashabiki wa West Ham wakilishambulia gari la Manchester United kwa makopo ya vinywaji kabla ya mchezo tukio ambalo lilisababisha mchezo huo kuchelewa kuanza.









Hakuna maoni:
Chapisha Maoni