KLABU ya Manchester United imemtangaza rasmi Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya, akirithi mikoba ya Mholanzi, Louis Van Gaal aliyeondolewa wiki iliyopita.
Kocha
huyo amesaini Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 45
na atapewa Pauni Milioni 200 kwa ajili ya ajili ya usajili kuelekea
msimu mpya.
Na
Mreno huyo ametua Man United kutokana na klabu hiyo kuvutiwa na wasifu
wake mzuri akiwa ameshinda mataji yote ya Ulaya na Ligi za Serie A ya
Italia, Ligi Kuu ya England na La Liga ya Hispania.
Benfica
ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza, ambako baada ya mechi 11, aliweka
rekodi ya ushindi wa asilimia 54.55 kabla ya kuhamia Uniao de Leiria.
Kocha Jose Mourinho akiwa na jezi ya Man United baada ya kutambulishwa rasmi kuwa kocha timu hiyo leo
Na baada ya mechi 20, akachukuliwa na Porto na huko ndiko rasmi umaarufu wake kama kocha ulipoibukia.
Ilimchukua
Mourinho misimu miwili tu kufanya ambacho hakikufikiriwa baada ya
kuwaongoza vigogo hao wa Ureno kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
wakiifunga Monaco ya Ufaransa kwenye fainali.
Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 53 baada ya mafanikio hayo akajipa 'Special
One' wakati anawasili Chelsea na akapata umaarufu zaidi baada ya
kushinda mataji katika misimu yake miwili ya mwanzo Stamford Bridge.
Pia
ameshinda mataji ya Kombe la FA na mawili ya Kombe la Ligi England,
lakini mmiliki wa Chelsea, bilionea Mrusi Roman Abramovich akamuondoa
kazini.
Mreno
huyo akahamia Serie A ambako akashinda taji katika msimu wake wa kwanza
kabla ya kuiongoza Inter Milan kutwaa mataji msimu uliofuata, likiwemo
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mourinho
akaenda kuwa kocha wa 11 wa Real Madrid ndani ya miaka saba na
kufanikiwa kuzima ubabe wa Barcelona kutwaa mfululizo mataji ya La Liga
kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Hispania, katika msimu wake wa pili.
Hakuweza
kutwaa taji la Ulaya na akashindwa kutwaa taji lolote katika msimu wake
wa mwisho na akaondoka kwa makubaliano mazuri, kabla ya kurejea Chelsea
ambako katika msimu wake wa kwanza akashika nafasi ya tatu kwenye Ligi
Kuu kabla ya kushinda taji hilo katika msimu uliofuata na kusaini
Mkataba mpya hadi mwaka 2019.
Lakini mwanzo wa msimu wa 2015-16 haukuwa mzuri kwa Mourinho baada ya kuandamwa na matokeo mabaya hadi akaondolewa
MATAJI ALIYOSHINDA MOURINHO
MATAJI ALIYOSHINDA MOURINHO
Porto (Mataji 6)
Januari 2002 - Mie 2004
Primeira Liga: 2002-03, 2003-04
Taca de Portugal: 2002-03
Supertaca Candido de Oliveira: 2003
UEFA Champions League: 2003-04
UEFA Cup: 2002-03
Chelsea (Mataji6)
Chelsea (Mataji6)
Juni 2004 - Septemba 2007
Premier League: 2004-05, 2005-06
FA Cup: 2006-07
League Cup: 2004-05, 2006-07
FA Community Shield: 2005
Inter Milan (Mataji 5)
Juni 2008 - Mei 2010
Serie A: 2008-09, 2009-10
Coppa Italia: 2009-10
Supercoppa Italiana: 2008
UEFA Champions League: 2009-10
Real Madrid (Mataji 3)
Mei 2010 - June 2013
La Liga: 2011–12
Copa del Rey: 2010–11
Supercopa de Espana: 2012
Chelsea (Mataji 2)
June 2013 - December 2015
Premier League: 2014-15
League Cup: 2014-15
Tuzo na mataji binafasi
Kocha Bora wa Mwaka wa Onze d'Or: 2005
Kocha Bora wa Dunai wa FIFA: 2010
Kocha Bora wa IFFHS: 2004, 2005, 2010, 2012
Kocha Bora wa Ligi Kuu England wa Mwaka; 2004–05, 2005–06, 2014–15
Kocha Bora wa Mwaka wa Serie A: 2008–09, 2009–10
Kocha Bora wa Mwaka wa UEFA: 2002–03, 2003–04
Timu Bora ya Mwaka ya UEFA: 2003, 2004, 2005, 2010
Kocha Bora wa BBC Sports Personality wa Mwaka; 2005
Mwanamichezo Bpra wa La Gazzetta dello Sport: 2010 Kocha Bora wa Karne wa Ureno: 2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni