Ndani ya dimba la Giusseppe Meazza (San Sirro) Jumamosi hii kutakuwa na vita ya kuuwania ufalme wa Ulaya baina ya watoto wa mji mmoja, Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid umbali wa km 15 za barabara unaweka tofauti ya kimakazi baina ya mahasimu hawa.
Wakati macho na akili za mamilioni ya mashabiki zikielekezwa katika kutaka kujua nani atakayeibuka na ushindi mwishoni mwa kipyenga cha mwamuzi Mark Clattenburg kutoka England.
Kocha wa Real Madrid,Zinedine Yazid Zidane ‘Zizzou’, ambaye ulimwengu mzima unaamini kuwa mchezaji aliyefunga goli bora zaidi la wakati wote katika michuano ya UEFA, pindi alipopigilia ‘volley’ iliyoipa Real Madrid ushindi wa taji lake la tisa la michuano hii mnamo mwaka 2002.
Anayo nafasi ya kuingia katika kumbukumbu ya kihistoria na kuwa mtu wa saba kuwahi twaa taji la Ulaya akiwa ndani ya jezi kama mchezaji na baadaye ndani ya suti ya ukocha.
Wataalamu wengine waliowahi kufanya hivyo ni
Giovanni Trapattoni (1963, 1969 akiwa mchezaji wa Ac Milan na 1985 akiwa kocha wa Juventus)
Carlo Ancelotti (1989, 1990 akiwa mchezaji wa Ac Milan na 2003, 2007-Ac Milan ,2014 akiwa kocha wa Real Madrid)
Johan Cruyff (1971, 1972, 1973 akiwa mchezaji wa Ajax na 1992 akiwa kocha wa Barcelona)
Frank Rijkaard (1989, 1990-Ac Milan, 1995 akiwa mchezaji wa Ajax na 2006 akiwa kocha wa Barcelona)
Pep Guardiola (1992 akiichezea Barcelona na 2009, 2011 akiifundisha Barcelona)
Miguel Muñoz,( 1955–56, 1956–57, 1957–58 akiichezea Real Madrid na 1959–60, 1965–66 akiwa kocha wa Real Madrid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni