STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 17 Mei 2016

RAISI WA SIMBA ATAJA "MAJIPU" KWENYE TIMU YAO MSIMU HUU, HATAREEE



RAIS wa Simba SC, Evans Aveva ametaja sababu kadhaa za timu hiyo kufanya vibaya msimu huu, mojawapo ni kuwa wachezaji wasio waaminifu baadhi yao beki Hassan Kessy na mshambuliaji Ibrahim Hajib.

http://www.mwanaspoti.co.tz/image/view/-/3021014/lowRes/1091567/-/5gepdb/-/pic+aveva.jpg Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo hoteli ya Collessium, barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, Aveva amesema wachezaji hao walifanya vitendo ambavyo vimewaondolea uaminifu katika klabu.

Aveva alisema Kessy alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu na baada ya adhabu hiyo, klabu ikaamua kumuongezea adhabu, lakini kabla hajamaliza adhabu zake akaibuka anasaini kwa mahasimu Yanga.

Kuhusu Hajib, Aveva alisema mshambuliaji huyo alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu pia na asubuhi yake akapanda ndege kwenda Afrika Kusini.

Amesema mambo kama hayo pamoja na uendeshwaji mbovu wa Ligi Kuu unaofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) vimechangia Simba SC kufanya vibaya msimu huu. 

Aveva amesema kutakuwa na Mkutano Mkuu wa klabu Julai 10, mwaka huu kujadili matatizo ya klabu na kutafuta suluhisho lake.

Aveva alisema shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limechangia kutokana na upangaji mbovu wa ratiba ambao umekuwa ukifanya baadhi ya timu kuwa nyuma kwa michezo minne kitu kinachorahisisha upangaji wa matokeo.

Rais huyo pia aliwataja waamuzi kuwa sababu ya Wekundu hao kukosa ubingwa msimu huu kwakua walionekana kuingia uwanjani wakiwa na matokeo mfukoni na ameishauri TFF katika mechi za watani wa jadi marefa watoke nje ya nchi ili haki ipatikane.

Aidha Aveva aliwataja waandishi wa habari kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro ndani ya Simba kutokana na kuripoti vibaya habari za klabu yake na kuwachochea mashabiki na wapenzi wa timu hiyo.

"Waandishi mmekuwa sehemu ya migogoro ndani ya Simba na kuna redio moja hapa mjini ndiyo inasababisha kwa kuwapigia watu wa nje kuzungumzia mambo muhimu ndani ya klabu" alisema Aveva.

Pia Aveva amewataja wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa kutochukua ubingwa kutokana na kutokuwa wavumilivu mpaka ikafika hatua wanalipiga mawe basi la timu na kumjeruhi mchezaji wetu.

"Katika mpira kuna matokeo matatu na wanajua lakini walitugeuka na kututukana kuwapiga viongozi na basi la Wachezaji sasa kwa mazingira hayo ubingwa utaupataje" alihoji Aveva .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox