Liverpool ambao waliunza
mchezo kwa kasi kipindi cha kwanza ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli
dakika ya 35 kupitia kwa Daniel Sturridge baada ya kupokea pasi kutoka
kwa Phillipe Coutinho.
Kipindi cha pili
kilipoanza mshambuliaji Kelvin Gameiro aliisawazishia Sevilla baada ya
kupokea pasi toka kwa Mariano huku magoli mengine yakifungwa na Coke
dakika ya 64 na 70.Pamoja na kupata magoli hayo, pia mabingwa hao wa kihistoria walionekana kucheza vizuri kwa muda mwingi kipindi cha pili na kuwafanya majogoo wa Anfield kushindwa kuwazuia wanapofika langoni kwao.
Sevilla imenyakua taji hilo mara nne ndani ya miaka 10 tangu 2006. Imechukua ubingwa huo mwaka 2006, 2014, 2015 na 2016.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni