YANGA
SC imefanikiwa kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka
Afrika licha ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Sagrada Esperanca jioni ya
leo Uwanja wa Esperanca mjini Dundo, Angola.
Kwa
matokeo, hayo Yanga inakwenda hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa
2-1, baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam, mabao ya Simon Msuva na
Matheo Anthony.
Matokeo
hayo si tu yanamaanisha Yanga inatinga hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia yake, bali pia inakuwa
timu ya kwanza ya Tanzania kufika hatua hiyo ya michuano hivyo.
Awali
ya hapo, Yanga imewahi kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufika hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998, ikafuatiwa na mahasimu,
Simba SC mwaka 2003.
Katika
mchezo wa leo uliochezeshwa na marefa wa Madagascar, Hamada el Moussa
Nampiandraza, aliyesaidiwa na Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean
Thierry Djaonirina, hadi mapumziko, tayari wenyeji walikuwa
wamekwishajipatia bao lao hilo.
Bao
hilo lilifungwa na mkongwe Arsenio Sebastiao Cabungula maarufu kama
‘Love Kabungula’ dakika ya 25, baada ya mabeki wa Yanga kufanya uzembe
kidogo.
Yanga
walitulia baada ya bao hilo, licha ya marefa kuonekana kabisa
kupendelea wenyeji na wakafanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa
nyuma kwa bao hilo moja tu.
Kipindi
cha pili, Yanga waliachana na mchezo wa kujihamia na kufunguka kuanza
kushambulia, hali ambayo ilipunguza kasi ya wapinzani wao.
Kocha Mholanzi alimtoa kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko baada ya kuumia na kumuingiza Deus Kaseke dakika ya 69.
Mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma alipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 72.
Winga
Simon Msuva alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 86 na dakika ya 89
kipa Deo Munishi 'Dida' akaokoa penalti iliyotolewa baada ya Nahodha,
Cannavaro kumuangusha mchezaji wa Sagrada Esperanca.
Refa
aliongeza dakika tano baada ya kutimia dakika 90 na Nahodha Cannavaro
akatolewa kwa kadi nyekundu pia dakiak ya 90 na ushei.
Vurugu
zikaibuka dakika ya mwisho ya dakika za nyongeza na kipa wa Yanga, Dida
akapigwa jiwe na mchezo kusimama kwa muda. Askari Polisi waliingia
uwanjani kutuliza fujo na mchezo ukaendelea kwa sekunde kadhaa kabla ya
refa kumaliza.
Ikumbukwe,
Yanga iliangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya
Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16
Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa
sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.
Yanga
ilianza vizuri tu kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla
ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na
APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare
ya 1-1 Dar es Salaam.
Kikosi
cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua,
Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva,
Thabani Kamusoko/Deus Kaseke dk69, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Kevin
Yondan dk90 na Haruna Niyonzima.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatano, 18 Mei 2016
Home
/
Unlabelled
/
YANGA YASONGA KIMATAIFA LICHA YA KUFUNGWA 1-0, FIGISU ZATAWALA NDANI NA NJE YA UWANJA
YANGA YASONGA KIMATAIFA LICHA YA KUFUNGWA 1-0, FIGISU ZATAWALA NDANI NA NJE YA UWANJA
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni