STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 10 Mei 2016

UNAKOSAJE RADHA HADIMU YA EPL KIPINDI HIKI CHA MWISHONI ?


 


Vita ya kushuka daraja, ‘top four’ ndipo utamu wa EPL ulipo WASWAHILI husema utamu wa jambo ukizidi basi tambua kwamba mwisho wake unakaribia. 

Nimeukumbuka msemo huo baada ya kuiangalia ratiba ya Ligi Kuu England maarufu kama EPL na kuona kila timu imebakisha mechi moja kumaliza msimu huu. 

Ndiyo ni mechi moja moja ukiondoa michezo ya leo Jumanne na kesho Jumatano.
 


 Siku zinaenda kasi, ukizubaa utashtuka huna chako, hiyo ndiyo imewakuta Aston Villa na sasa inasubiri kukamilisha ratiba na msimu ujao ishiriki Ligi Daraja la Kwanza. 

Msimu huu wa 2015/16, Jumapili hii unafikia tamati kwa timu zote 20 kupambana kwenye viwanja kumi tofauti kusaka pointi za heshima. Tayari bingwa wa ligi hiyo kashakabidhiwa kombe lake. 

 http://i1.mirror.co.uk/incoming/article7920841.ece/ALTERNATES/s615b/Leicester-City-lift-the-Premier-League-trophy.jpg

Leicester City ndiyo iliyotwaa taji hilo msimu huu wakiwa wamebakiwa na michezo miwili mkononi. Leicester imechukua taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Chelsea. 

Kwa sasa vita imebaki katika nafasi hizi mbili, kushuka daraja na nyingine ile ya kumaliza ndani ya nafasi nne za juu. Kama nilivyosema hapo awali, tayari Aston Vila imeshashuka daraja huku Leicester na Tottenham Hotspur ‘Spurs’ zenyewe zikiwa na uhakika wa kumaliza top four.

 Kwa sasa Leicester ndiyo mabingwa na Spurs inashika nafasi ya pili. Spurs inahitaji pointi moja tu ili kujihakikishia kubaki katika nafasi yake hiyo ya sasa. 

Mchezo wao wa mwisho Spurs watacheza dhidi ya Newcastle, mchezo huu unaweza kuwa mkali kwa maana kwamba Spurs wanataka pointi moja tu kuitetea nafasi yao huku Newcastle wakihitaji pointi zote tatu ili kujinasua na janga la kushuka daraja. 
 

Newcastle yenye pointi 34 baada ya kucheza michezo 37, inashika nafasi ya tatu kutoka mkiani na inazihitaji zaidi pointi hizo huku ikiziombea njaa Sunderland na Norwich ambazo zote zimebakiwa na michezo miwili.

 Kesho Jumatano Sunderland itapambana na Everton huku Norwich ikicheza dhidi ya Watford. Sunderland inashika nafasi ya nne kutoka mkiani, ina pointi 35 baada ya kucheza mechi 36 msimu huu mpaka sasa. Norwich ambayo yenyewe inashika nafasi ya pili kutoka mkiani, ina pointi 31 baada ya kucheza michezo 36 msimu huu.

 http://fullhdpictures.com/wp-content/uploads/2015/10/Excellent-Sunderland-Wallpaper.jpg

 Kama timu hizo mbili zikishinda michezo yao ya Jumatano hii, ni wazi Newcastle itakuwa na wakati mgumu wa kubaki ligi kuu kwa msimu ujao. Kwa jinsi hali ilivyo, Sunderland inaonekana ina nafasi kubwa ya kusalia ligi kuu kwani kama ikishinda mchezo wa kesho, basi kazi itakuwa imekwisha.

 Sunderland na Norwich zitakuwa zimeungana na Aston Villa kushuka daraja bila ya kusubiri michezo ya wikiendi hii, hapo ndipo Waswahili husema ulichokipanda ndicho utakivuna.

 

Ratiba za michezo yao ya kumaliza msimu ipo hivi; Mei 11, 2016 Sunderland v Everton Norwich v Watford Mei 15, 2016 Watford v Sunderland Newcastle v Spurs Everton v Norwich Arsenal v Aston Villa .

 Msimamo mkiani upo hivi;

                         P GD Pts 
17. Sunderland 36 -17 35 
18 .Newcastle  37 -25 34 
19 .Norwich     36 -27 31 
20 .Aston Villa 37 -45 17 

Tukifungua ukurasa wa pili ambapo kuna hadithi tamu ambazo si zile za abunuasi, bali hizi tunazifananisha na za Sungura na Fisi. 

Kama wewe utotoni kwako ulikuwa unapenda kukaa beneti na bibi au babu yako bila shaka ushawahi kusikia japo hadithi tatu au nne zinazowahusu sungura na fisi. 

Sungura na fisi ni wanyama wanaosemekana kuwa ni marafiki sana lakini ndiyo wanaongoza kwa kusalitiana linapokuja jambo la kimaslahi.
 


 Ukiangalia katika msimamo huo wa EPL, timu za Arsenal, Manchester City na Manchester United zinafukuzia kumaliza ligi zikiwa ndani ya ‘top four’ ili msimu ujao ziweze kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Arsenal inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 68, imebakiwa na mchezo mmoja. Man City inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 65 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi. 

Man United inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 63, yenyewe imebakiwa na michezo miwili mkononi ambayo kama ikishinda yote na timu zilizokuwa juu yake zikapoteza michezo yao ya mwisho, basi United itamaliza ikiwa ya tatu. 




Kabla ya michezo ya mwisho, United inahitaji zaidi kushinda mchezo wao wa leo Jumanne dhidi ya West Ham United. Baada ya mchezo huo, United itamaliza dhidi ya Bournemouth ambayo haina cha kupoteza baada ya kuepuka kushuka daraja.

 Arsenal inahitaji pointi moja tu kumaliza ligi ikiwa ya tatu, katika mchezo wake wa mwisho itapambana dhidi ya Aston Villa ambayo tayari tunaweza kusema ni maiti inayotembea nikiwa na maana kwamba timu hiyo imeshakufa katika vita ya ligi kuu na sasa inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, lakini hiyo haiwezi kuwafanya kuwa wanyonge, naamini watapambana ili tu washinde mchezo huo wa mwisho ili kulinda heshima yao.

 Man City yenyewe itamaliza ligi kwa kucheza dhidi ya Swansea. Mechi za timu hizo zote zinazowania nafasi nne za juu zitachezwa katika viwanja vyao vya nyumbani kasoro Man City pekee ambayo itacheza ugenini. 
 


Mcheza kwao hutuzwa, Arsenal, Man United zitajivunia kuwa nyumbani huku Man City wakiingia ugenini na kauli kwamba mgeni lazima akarimiwe, hivyo watataka kuona ukarimu wa Swansea upoje katika kuwapa pointi. Huku tukiwa tunaiangalia vita hiyo, nakiona kituko kinaweza kutokea. 

Shirikisho la Soka Ulaya limebadilisha baadhi ya kanuni zake za mashindano, na sasa inaipa nafasi timu kutoka taifa fulani kucheza michuano hiyo mikubwa barani humo kwa ngazi ya klabu hata kama imekosa kumaliza kwenye zile nafasi za juu kwenye ligi ya nyumbani kwao, sharti ni kwamba ikichukua ubingwa wa Europa League tu moja kwa moja inacheza Ligi ya Mabingwa.
 


Kwa England, Liverpool ambayo kwa sasa inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 58 ambazo hata kama ikishinda michezo yake miwili haiwezi kumaliza ndani ya ‘top four’, lakini ndiyo inacheza fainali ya Europa League. 

Hivyo basi Liverpool itafanya jitihada kuhakikisha inabeba taji hilo ili kucheza Ligi ya Mabingwa na hiyo itaacha majonzi kwa timu itakayomaliza nafasi ya nne kwani italazimika kushiriki Europa League.

 Liverpool ikifanya hivyo, itatukumbusha msemo unaosema hivi, “mlango wa uani nao ni mlango japo hauna heshima.”

 Msimamo kwa timu za juu upo hivi ;

                     P GD Pts 
1 Leicester    37 32 80 
2 Spurs         37 38 70 
3 Arsenal      37 25 68
 4 Man City   37 30 65 
5 Man Utd    36 13 63

Email;mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox