CHILE KUCHEZA NA MABINGWA WA EURO 2016.
MABINGWA wa michuano ya
Copa America, Chile wanatarajiwa kupambana na bingwa wa michuano ya
Ulaya anakayepatikana baadae mwezi ujao.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na rais wa Shirikisho la Soka la America Kusini-CONMEBOL,
Alejandro Dominguez, mchezo huo utakaokutanisha bingwa wa Copa America
na Euro 2016 utachezwa katika miezi michache ijayo.
Wakati Chile
wakijihakikishia nafasi yao ya kushiriki Kombe la Shirikisho mwaka 2017,
Dominguez amebainisha kuwa tayari wameshatuma barua ya maombi ya mchezo
huo kwa Shirikisho la Soka la Ulaya.
Dominguez amesema mara baada ya
kutuma barua hiyo wamepata majibu ya matumaini kwamba mchezo huo unaweza
kuwepo hivyo wanachotakiwa kufanya ni kutafuta tarehe itakayofaa.
HULK AKAMILISHA USAJILI WAKE CHINA.
Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu
ya China-CLS imelipa kitita cha euro milioni 56 kwa mchezaji huyo
ambachi kimeweka rekodi mpya ya usajili katika ligi hiyo.
Zenit pia
wanatarajiwa kupata bakshishi ya euro milioni mbili zaidi kama
mshambuliaji huyo atafunga mabao zaidi ya 15.
Inadaiwa kuwa Hulk
amekubalia mshahara wa euro milioni 12.5 kabla ya bakshishi, kiasi
ambacho kitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi CLS.
Klabu hiyo
ilithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wake na kudai kuwa Hulk
alisaini mkataba wake pindi alipomaliza vipimo vyake vya afya.
SCOLARI ATAMANI KUINOA UINGEREZA.
KOCHA wa zamani wa
Brazil, Luiz Felipe Scolari ametangaza nia yake ya kuja kuwa meneja
ajaye wa timu ya taifa ya Uingereza.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67
ambaye aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002, alipata
nafasi ya kuchukua mikoba ya Sven-Goran Eriksson kama meneja wa
Uingereza mwaka 2006 kabla ya kujitoa kutokana na kushambuliwa na vyombo
vya habari vya nchi hiyo.
Scolari ambaye alishindwa kupata mafanikio
katika klabu ya Chelsea kwa kutimuliwa baada ya miezi sita, amesisitiza
kuwa yuko tayari kwa chochote ambacho Chama cha Soka Uingereza
kitahitaji kutoka kwake kama akiteuliwa kuwa kocha.
Akihojiwa Scolari
amesema kwasasa yeye bado ni meneja wa Guanghou na anakipenda kibarua
chake lakini anafahamu umuhimu wa kibarua cha kuinoa Uingereza katika
ulimwengu wa soka hivi sasa.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anahusudu
soka la Uingereza na anafahamu mahitaji ya timu ya taifa kuwa inahitaji
mafanikio.
SIMEONE ASISITIZA KUENDELEA KUBAKIA ATLETICO.
MENEJA wa Atletico
Madrid, Diego Simeone amefafanua kauli yake aliyoitoa kufuatia timu yake
kupoteza mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi
uliopita.
Atletico ilishindwa kutamba kwa mara ya pili katika kipindi
cha miaka mitatu baada ya kutandikwa tena mahasimu wao wa jiji Real
Madrid.
Baada ya mchezo huo ambao walipoteza kwa changamoto ya mikwaju
ya penati jijini Milan, Simeone amesema anatarajiwa kuchukua muda
kufikiria kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo.
Lakini meneja huyo
mwenye umri wa miaka 46 amesema kauli hiyo aliitoa wakati akiwa katika
kipindi kibaya, kwani hana mpango wowote wa kuondoka Atletico
kwasasa.
Simeone aliendelea kudai kuwa Atletico itaendelea kuwa moja ya
vikosi bora kabisa katika ulimwengu wa soka katika miaka mingi
ijayo.
Meneja huyo amesema timu pekee zinazowazidi kwa ubora ni
Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich, hakuna nyingine.
NOLITO ANUKIA CITY.
WINGA mahiri wa
kimataifa wa Hispania, Nolito anadaiwa kuwa tayari ameshatua jijini
Manchester kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester
City.
Nyota huyo anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kusajili na meneja
mpya wa klabu hiyo Pep Guardiola baada ya kufikia makubaliano mabo
binafsi na timu hiyo ya Ligi Kuu.
Nolito anatarajiwa kumalizia baadhi
vitu vichache vilivyobaki katika uhamisho wake kutoka Celta Vigo ambao
umegharimu kiasi cha paundi milioni 14, pindi atakapotembelea kituo cha
michezo cha City.
Mara baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya,
Nolito anatarajiwa kutembezwa katika kituo hicho kabla ya kupigwa picha
na kutambulishwa rasmi kwa vyombo vya habari.
Nyota huyo atakuwa mchzaji
pili kusajiliwa na City baada ya Ilkay Gundogan aliyesajiliwa kutokea
Borussia Dortmund Juni 2 mwaka huu.
NEYMAR KUJITIA KITANZI
BARCELONA.
RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema Neymar anatarajiwa
kusaini mkataba mpya katika kipindi cha siku chache zijazo. Mkataba wa
sasa wa neymar unamalizika Juni mwaka 2018 na mazungumzo ya mkataba mpya
yamekuwa yakindelea kwa muda sasa hivyo kuzusha tetesi kuwa klabu za
Real Madrid, Paris Saint-Germain au Manchester United zinaweza kulipa
kitenzi cha euro milioni 200 kilichowekwa katika mkataba wake. Hata
hivyo, akiongeza na wanahabari mapema leo, Bartomeu amesema Neymar
hatakwenda popote na katika siku chache zijazo atasaini mkataba mpya wa
miaka mitano zaidi. Wakala wa zamani wa Neymar, Wagner Ribeiro hivi
karibuni alidai kuwa kuna klabu tatu kubwa zinazomfukuzia nyota huyo wa
kimataifa wa Brazil lakini mwenyewe anafurahia kuendelea kubakia Camp
Nou. Neymar alijiunga na Barcelona akitokea Santos mwaka 2013 a
kufanikiwa kushinda taji la La Liga na Kombe la Mfalme mara mbili pamoja
na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana.
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni