June 21 2016 jina la nahodha wa timu ya taifa ya Sweden aliyekuwa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika.
Zlatan amefikia maamuzi hayo ikiwa ni siku chache zimepita toka atangazwe katika list ya wachezaji wa Sweden watakaoicheza michuano ya Olympic Brazil, hizi zinatajwa kuwa ni habari njema wa Man United ambao wanatajwa kuwa watamsajili baada ya Euro, kwani atakuwa huru na muda mwingi zaidi wa kuitumikia klabu yao.
Nahodha huyo wa Sweden ameanza kucheza timu ya taifa toka 1999 akiwa timu za vijana na mwaka 2001 ndio alianza kucheza timu ya wakubwa “
Mechi hizi za Euro 2016 ndio zitakuwa za mwisho mimi kuichezea Sweden, ni heshima kuwa nahodha wa Sweden kwa kipindi chote, popote nitakapoenda nitakuwa na bendera ya Sweden kwa sababu mimi ni msweden”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni