Jina la Lionel Messi
sio jina geni katika masikio ya wapenda soka wengi, hii inatokana na
uwezo wake mkubwa wa kucheza soka na kuweka na kuvunja rekodi mbalimbali
za mchezo wa soka, alfajiri ya June 22 2016 Lionel Messi amerudi tena kwenye vichwa vya habari baada ya kuvunja rekodi nyingine katika mchezo wa nusu fainali waliyoshinda na kutinga fainali ya Copa America 2016.
Lionel Messi amefanikiwa kuvunja rekodi ya ufungaji wa muda wote katika timu ya taifa ya Argentina, amefunga jumla ya magoli 55 baada ya kufunga goli la dakika ya 32 katika ushindi wa magoli 4-0 nusu fainali ya Copa America 2016 dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo USA, awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na mkongwe wa Gabriel Batistuta.
Batistuta hadi anastaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina alikuwa kaifungia magoli 54, rekodi ambayo imevunja na Lionel Messi aliyefunga jumla ya magoli 55 na kuwa ndio mfungaji bora wa Argentina wa muda wote, magoli ya Argentina yalifungwa na Lavezzi dakika ya 4, Lionel Messi dakika ya 32 na Higuan dakika ya 50 na 86.
VIDEO MAGOLI YA ARGENTINA;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni