Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye
kwasasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Paris Saint-Germain
kumalizika amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda United na
China.
Ibrahimovic aliwaambia wanahabari leo kuwa atabainisha klabu
atakayokwenda pindi atakapochoka kusoma tetesi nyingi
zilizozagaa.
Mkongwe huyo aliwahi kuichezea Malmo ikiwa ndio klabu yake
ya kwanza kuanzia mwaka 1996 mpaka 2004.
Baadae akaenda kuzichezea klabu
za Ajax Amsterdam, Juventus, Inter Milan, Barcelona na AC Milan kabla
ya kujiunga na PSG mwaka 2012.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni