Baada ya mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Copa America kati ya Chile dhidi ya Colombia kusimama kwa zaidi ya saa moja, hatimae uliendelea na kupatikana kwa mshindi atakayecheza mchezo wa fainali dhidi ya Argentina Jumapili ya June 26 2016 katika uwanja wa MetLife.
Colombia licha ya
mchezo kusimama na wao kupata nafasi ya kupumzika vya kutosha na
kushauriana, walishindwa kuchomoa goli 2-0 zilizokuwa zimefungwa kipindi
cha kwanza dakika ya 7 na Charles Aranguiz na Jose Fuenzalida dakika ya 11.
Argentina atacheza na Chile katika fainali lakini nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa Copa America anapewa Argentina kutokana na rekodi yao ndani ya miaka 106 Argentina kapoteza mechi 7 peke dhidi ya Chile, wakati Argentina amewahi kumfunga Chile kwa zaidi ya mara 40 huku mwaka uliopita Chile akimfunga Argentina katika mashindano haya na kuchukua ubingwa katika fainali.
Magoli yalioipeleka Chile fainali ya Copa America 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni