KAMPUNI
ya Bin Slum Tyres Limited kupitia betri zake maarufu za RB, leo
imeongeza Mkataba wa udhamini na klabu ya Mbeya City FC ya Mbeya.
Zoezi
hilo limefanyika mchana wa leo katika hafla maalum fupi iliyofanyika
kwenye ofisi za Bin Slum Tyres Limited, Lumumba, Dar es Salaam.
Akizungumza
baada ya kukamilisha zoezi hilo, Naibu Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres
Limited, Mohammed Bin Slum alisema kwamba wameamua kuiongezea Mkataba
klabu hiyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
Mohammed, kiungo wa zamani wa Coastal Union ya Tanga amesema Mkataba mpya na utakuwa na thamani sawa na Mkataba wa awali.
“Tunayo
furaha kuongeza Mkataba na Mbeya City baada ya ule wa awali kumalizika
na tumefanya hivi baada ya kuvutiwa na mwenendo wao mzima,”amesema Bin
Slum.
Katika
hafla hiyo, Mkurugenzi huyo pia aliwakabidhi vifaa vya michezo vya
msimu mpya, vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 50 ikiwa ni pamoja na
seti tatu za jezi.
Kwa
upande wake, Meya wa Manispaa ya Mbeya, David Polela Mwashilindi
aliwashukuru Bin Slum kwa kuiteua Mbeya City kati ya timu nyingi za
Tanzania na kusema wataendelea kuiwakilisha vyema kampuni hiyo.
Katibu
wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amewashukuru Bin Slum Tyres kwa kuendelea
kuwadhamini na akaahidi watalipa fadhila kwa kutwaa taji msimu ujao.
“Tutajitahidi
msimu ujao tulete Kombe lolote hapa, ili kulipa fadhila kwa udhamini
huu, kama si la Ligi Kuu basi Kombe la TFF, tutakuletea hapa,”alisema
Kimbe kumuambia Bin Slum.
Bin
Slum Tyres Limited iliingia Mkataba na Mbeya City kwa mara ya kwanza
mwaka 2014 ikiwapa dau la Sh. Milioni 360, yaani Sh. Milioni 180 kwa
mwaka.
Fedha hizo ni nje ya vifaa vya michezo wanavyopewa kila mwaka, ambavyo ni pamoja na seti tatu za jezi za kisasa kila msimu.
Na
mwaka jana Bin Slum Tyres Limited iliwakabidhi Mbeya City basi jipya
kubwa la kisasa lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 200.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni