MECHI kati ya Yanga SC na TP Mazembe ya DRC Jumanne ijayo itachezwa kuanzia Saa 10:30 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alipozungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam.
Muro amesema kwamba mpango wa kuipeleka mechi hiyo usiku umeshindikana kutokana na Jenereta la Uwanja wa Taifa kuwa bovu kwa sasa.
Yanga itawakaribisha Mazembe Jumanne ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huo ukiwa mchezo wa pili wa Kundi A, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
Jenereta la Uwanja wa Taifa ni bovu kwa sasa hivyo mechi zinachezwa mchana tu |
Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
Kikosi cha Yanga kimeweka kambi mjini Antalya, Uturuki na kinatarajiwa kurejea nchini kesho usiku kwa maandalizi ya mwisho.
Kikosi kamili cha Yanga kilichopo kambini Uturuki ambacho kinatarajiwa kurejea Ijumaa usiku ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
Mabeki; Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Vincent Bossou na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya na Obrey Chirwa.
Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.
Msafara upo chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni