KLABU ya Simba inatarajiwa kumtangaza Meneja wa zamani wa
Azam FC, Patrick Kahemele kuwa Mtendaji wake Mkuu.
Aidha, Simba inatarajiwa kumtangaza kocha wa zamani wa Azam FC, Mcameroon, Joseph Marius Omog kuwa kocha mpya Mkuu wa klabu hiyo.
Kikao
cha Kamati ya Utendaji ya Simba kilitarajiwa kupokea pendekezo la kuajiriwa kwa
Kahemele kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu usiku wa kuamkia leo pamoja na Omog kuwa kocha Mkuu.
Na kutokana na Kahemele kuungwa mkono na Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji, baada ya kazi nzuri aliyowahi kuifanya akiwa Azam FC – kuna matarajio makubwa dili hilo litafanikiwa.
Akizungumza usiku wa jana, Kahemele amesema kwamba
amefanya mazungumzo na uongozi wa Simba na kufikia makubaliano, lakini bado
hajapewa Mkataba.
“Ni kweli, nimefanya mazungumzo na uongozi wa Simba, na kimsingi tumefikia makubaliano ila bado hatujaingia Mkataba,”amesema.
Pamoja na hayo, habari zaidi zinasema Kahemele amewasaidia Simba SC kumpata kocha wa zamani wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog.
“Kahemele ni kiongozi wa kisasa kabisa, mweledi,
mchapakazi na mbunifu. Tunaamini atarudisha heshima ya Simba. Hapa hajaanza
kazi, lakini ametusaidia vizuri katika mchakato wa kupata kocha,”kimesema
chanzo kutoka Simba.
Simba imekuwa haina kocha Mkuu tangu Januari mwaka huu alipoondoka Muingereza, Dylan Kerr mara baada ya kuajiriwa Kocha Msaidizi, Mganda Jackson Mayanja ambaye sasa atafanya kazi chini ya Omog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni