STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 25 Juni 2016

VIINGILIO GEMU YA YANGA HADHARANI WAKATI HUO WAREJEA KWA MAFUNGU.....................

 

YANGA SC imetaja viingilio viwili tu katika mchezo wake wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam mchana wa leo, Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema viingilio hivyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP.

 
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu mjini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo ambao utaanza Saa 10:00 jioni.
 
Jerry Muro (kushoto) akizingumza na Waandishi wa Habari leo Jangwani. Kulia ni Meneja Masoko, Omar Kaaya

Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

 
Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.


 WAKATI HUO;

 MSAFARA wa kwanza wa Yanga umerejea Dar es Salaam Alfajiri ya leo kutoka Antalya, Uturuki, walipokuwa wameweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne.
 
Yanga watakuwa wenyeji wa mabingwa wa mara tano Afrika, TP Mazembe Jumanne kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa pili wa Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika.

 
Na msafara wa kwanza umewasili Alfajiri, wakati kundi lingine litawasili usiku wa leo na kesho kikosi kizima kitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mazoezi.



Baadhi ya nyota wa Yanga waliokuwa kambini Uturuki, kutoka kulia ni Simon Msuva, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke
Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
 
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

 
Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.



Ukuta; Kutoka kulia kipa Deo Munishi 'Dida' na mabeki Vincent Bossou na Kevin Yondan 






































Kikosi kamili cha Yanga kilichokuwa kambini mjini ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
 
Mabeki; Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Vincent Bossou na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya na Obrey Chirwa.

 
Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.

 
Msafara upo chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh. 






























Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit (kulia) akiandika jezi na vifaa vingine vya michezo walivyokabidhiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  makao makuu ya shirikisho hilo, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho la Soka Afrika
Binzubeiry

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox