BEKI wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent 'Dante'amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC leo hii.
Vincent,
mmoja wa mabeki wa kati waliofanya vizuri msimu huu amesaini muda mfupi
baada ya kusiani kipa wa Prisons, Beno Kakolanya leo.
Dante
sasa anakwenda kupambana kugombea namba dhidi ya mabeki wengine wa kati
wa Yanga, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondan, Pato Ngonyani
na Mtogo Vincent Bossou.
Kakolanya
pia amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme hao wa soka ya
Tanzania, Yanga SC, jambo ambalo ni pigo kwa mahasimu, Simba SC
waliokuwa wanamtaka kipa huyo.
Kakolanya
anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’,
Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa
wanne.
Hata
hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa
Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo
Academy.
Picha Bin Zubeir
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni