STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 6 Juni 2016

YANGA WAIPIGA BAO LA KISIGINO SIMBA NI KWENYE MCHAKATO WA USAJILI, YANASA KIFAA...

KIPA wa Prisons ya Mbeya, leo Benno Kakolanya  amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme wa soka ya Tanzania, Yanga SC.

Usajili huo ni pigo kwa Simba SC ambao pia walikuwa wanamtaka kipa huyo, lakini ‘Chelewa Chelewa, mwana si wao tena” – kwani wenye kisu kikali wamefanya yao. 
 
Akizungumza na chombo kimoja cha habari leo, Kakolanya amesema kwamba amesaini Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka mitatu Prisons ya Mbeya.

“Nimesaini miaka miwili kujiunga na Yanga, baada ya kumaliza Mkataba wangu Prsons,”amesema kakolanya ambaye ni kipa wa tatu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.

Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo Academy.

Chanzo: Bin Zubeir

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox