STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 28 Juni 2016

YANGA WALITOA KIASI HICHI CHA FEDHA MASHABIKI WAINGIE BURE........

 

 

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka nchini (TFF), limeitaka Yanga kulipa fidia ya gharama za mchezo wake na TP Mazembe Sh milioni 530.

CAF na TFF imefikia hatua hiyo baada ya Yanga kufuta kiingilio katika mchezo wao huo wa makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na sasa mashabiki wataingia bure.

 

 

caf

 

 

Katika kikao chao cha jana kilichofanyika kwenye hoteli ya Coral Beach jijini na kukutanisha maofisa wa CAF, uongozi wa TFF, Polisi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na viongozi wa Yanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdetit wametakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kama gharama za mchezo.

 IMG-20160628-WA0009

Makato katika mchezo huo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho asilimia 15 ya fedha hizo zitaenda CAF, asilimia 15 nyingine gharama ya uwanja, TFF asilimia tano, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), asilimia 10, na Chama cha soka Dar es Salaam (DRFA) asilimia tano.

Tayari Yanga ilikuwa imechapisha tiketi 31,000 ambazo zingeuzwa kwa Sh7,000 ambazo zingeingiza Sh 217,000,000 huku zile za Sh 25,000 zilikuwa zimechapishwa tiketi 8,200 zingeingiza Sh milioni 205 huku VIP zilikuwa tiketi 5,000 ambazo zingeingiza Sh milioni 150 jumla ya fedha zote ambazo zingepatikana katika mchezo huo ni Sh milioni 572.

Pia Yanga wametakiwa kuingiza mashabiki wasiozidi 40,000 wakizidi kiwango hicho mchezo huo utafutwa na Yanga watalazimika kuwajibishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox