STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 19 Juni 2016

YANGA YAANZA VIBAYA KIMATAIFA, YACHAPWA ALGERIA NA WAARABU, NAFASI BADO IPO LAKINI..

YANGA SC imeanza vibaya mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kufungwa bao 1-0 wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia usiku wa kuamkia leo.

Shujaa wa MO Bejaia alikuwa ni beki Yassine Salhi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 20, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Ismail Belkacemi.

Matokeo hayo yanaifanya MO Bejaia ishike nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ambayo iliifunga Medeama ya Ghana 3-1 katika mchezo wa kwanza mjiji Lubumbashi Jumapili, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu.

Mechi zijazo za kundi hilo, Yanga watakuwa wenyeji wa Mazembe Dar es Salaam na Medeama wataikaribisha Mo Bejaia. 


Kikosi kamili cha Yanga kinachoanza ni; Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Twite, Oscar Joshua/Mwinyi Hajji dk33, Kelvin  Yondani, Vicent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Matheo Anthony dk85 na Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk75.


MO Bejaia; C. Rahmani, A. Messaoudi, A. Lakhdari, S. Baouali, S. Khadir, Y. Salhi/ M. Betorangal dk71, S. Benali, S. Sidibé, M. Ferhat/A. Mouhli dk87, M. Athmani na I. Belkacemi/ B. Bendjelloul dk79.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox