Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris.
Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa.
Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.
Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.
Matukio katika namba
35: Ureno wameshinda taji lao la kwanza la Ulaya baada ya mechi 35 kwenye mashindano hayo.
10: Ureno ni taifa la kumi tofauti kushinda kombe la mataifa ya Ulaya.
6: Eder ni mchezaji wa sita kufunga goli kwenye michuano ya Ulaya akitoea benchi anaungana na Oliver Bierhoff, Sylvain Wiltord, David Trezeguet, Juan Mata pamoja na Fernando Torres.
3: Ureno imekuwa nchi ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya kucheza mechi tatu hadi dakika 30 za nyongeza ndani ya msimu mmoja wa mashindano.
80: timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kupiga shuti lake on target dakika ya 80, muda mrefu zaidi kwenye fainali za michuano ya Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni