Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika
Julai 17 mwaka huu.
Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo
itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za
michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka kwa
wadhamini (Vodacom na Azam Tv).
Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa
tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora
wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora
wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.
Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo ya
mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul
(Yanga) na Mohamed Hussein (Simba) wakati kwa upande wa kipa bora ni
Aishi Manula (Azam), Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius
Munishi (Yanga).
Kocha bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky
Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).
Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi ni Farid Mussa
(Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza
Kichuya (Mtibwa Sugar).
Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora
wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent
Agban (Simba). Waamuzi bora katika kinyang'anyiro hicho ni Anthony
Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu
amewapongeza wateule wote waliopendekezwa kuwania tuzo hizo. "Kama
wadhamini tuna matumaini makubwa kuwa msisimko wa ligi hii utazidi
kuongezeka katika msimu ujao na kuzidi kuwapatia mashabiki wa soka
wanaoifuatilia hapa nchini na nje ya nchi."
Alisema Vodacom itaendelea kudhamini ligi hiyo
kubwa ya soka nchini ili kutekeleza moja ya malengo yao ya kuibua na
kuendeleza vipaji vya wachezaji nchini. Pia kuwawezesha wachezaji
kujipatia ajira na kuboresha maisha yao kupitia sekta ya michezo bila
kusahau kuwapatia burudani wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumamosi, 9 Julai 2016
Home
/
Unlabelled
/
KICHUYA, NGOMA, TSHABALALA, KAMUSOKO, MEXIME, FARID MUSSA, DIDA NA WENGINE KUWANIA TUZO ZA VPL JULAI 17
KICHUYA, NGOMA, TSHABALALA, KAMUSOKO, MEXIME, FARID MUSSA, DIDA NA WENGINE KUWANIA TUZO ZA VPL JULAI 17
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni