Premier
Legue iliwakilishwa na wachezaji wengi kwenye michuano ya Euro 2016
huko Ufaransa lakini katika hatua ya fainali wamesalia wachezaji 12
pekee kutoka kwenye ligi hiyo yenye watazamaji lukuki duniani.
Yamebaki
mataifa mawili hadi sasa ambayo yatacheza fainali ya Euro 2016, wenyeji
Ufaransa ambao walifika hatua ya fainali siku ya Alhamisi usiku baada
ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya washindi wa Kombe la Dunia Ujerumani,
watakabiliana na Ureno siku ya Jumapili usiku.
Vilabu
nane vya Premier League vitawakilishwa na wachezaji wao kwenye hatua
hii huku Manchester United na wapinzani wao wa karibu Manchester City
wakiwakilishwa na wachezaji wao wawili kama ilivyo kwa Arsenal pia.
Kuna
utitiri wa wachezaji wa Premier League kwenye kikosi cha Ufaransa
wakati huo ukimtoa kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko ambaye timu yake
imeshuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita 2015/16 na itacheza
Championship.
Kukiwa
na wachezaji 12 wa Premier League, 10 kati yao wanacheza kwenye timu ya
taifa ya Ufaransa wakati wawili wanaiwakilisha Southampton watakuwa
wakiitetea Ureno.
Hapa kuna list ya wachezaji wa Premier League waliotinga fainali ya Euro 2016:
Ureno:Jose Fonte-Southampton
Cedric Soares-Southampton
Ufaransa:
Hugo Lloris-Tottenham Hotspur
N’Golo Kante-Leicester City
Yohan Cabaye-Crystal Palace
Dimitri Payet-West Ham United
Olivier Giroud-Arsenal
Anthony Martial-Manchester United
Morgan Schneiderlin-Manchester United
Eliaquim Mangala-Manchester City
Bacary Sagna-Manchester City
Laurent Koscielny-Arsenal
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni