HABARI MCHANGANYIKO ;
Ligi kuu ya Hispania inatarajiwa
kuanza Agosti 21 kwa Mabingwa Watetezi FC Barcelona kucheza na Real
Betis na Mabingwa wa Ulaya Real Madrid kuanza na Real Sociedad, Vigogo
hao Wiki ijayo wanatarajiwa kurejea Mazoezini kujitayarisha na Msimu
mpya.
Jumatatu Barcelona watajumuika kuanza Mazoezi ya Wiki moja na kisha
kwenda England kupiga Kambi kwenye Kituo cha Mazoezi cha Timu ya Taifa
ya England St. George's Park.
Wakiwa huko England, Barca watacheza Mechi 3 dhidi ya Celtic, Leicester na kumalizia na Liverpool katika dimba la Wembley na kisha kurejea kwao kushiriki Kombe lao la Gamper Trophy dimba la Camp Nou na baada ya hapo wana Mechi 2 za nje na ndani kugombea taji la Supercopa dhidi ya Sevilla.
Katika maandalizi hayo Barcelona itawakosa Wachezaji kadhaa waliokuwa michuano ya ya EURO 2016 na Copa America Centenario wakiwemo wachezaji Neymar na Rafinha, ambao wataiwakilisha Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki itakayochezwa huko huko Brazil.
WAKATI HUO;
KLABU za Barcelona na Real Madrid zinatarajiwa kukutana Desemba katika ratiba mpya ya msimu wa 2016-2017 wa La Liga iliyotolewa leo.
Madrid waliomaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga nyuma ya Barcelona msimu uliopita, watasafiri kwenda Camp Nou katika wikiendi ya Desemba 3 au 4 ukiwa ni mchezo wao wa mwisho kwa la Liga kabla ya kusafiri kwenda kushiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia nchini Japan wakiwa kama mabingwa wa Ulaya.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 8 na kumalizika Desemba 18 mwaka huu.
Mechi ya marudiano kati ya mahasimu hao wa La Liga inatarajiwa kufanyika Santiago Berbabeu kati ya Aprili 22 au 23 mwakani.
TAARIFA KUTOKA FIFA
Shirikisho la soka Ulimwenguni
(FIFA) limetoa Ratiba ya Kombe la Dunia kwa Klabu ambalo litadhaminiwa
na Alibaba E-Auto na kufanyika huko Japan kati ya Desemba 8 na
18.
Mashindano haya yatashindaniwa na Klabu 6 Mabingwa wa Mabara pamoja
na Mwakilishi kutoka Nchi Mwenyeji Japan.
Hadi sasa Klabu 3 zimeshathibitika kucheza michuano hiyo ambazo ni Real Madrid, Mabingwa wa Ulaya, waliotwaa Ubingwa wao Mwezi Mei, na Timu nyingine ni Club America ya Mexico na Auckland City FC ya Mexico Bara la Oceanic ambazo zilitwaa Ubingwa wao Mwezi Aprili.
KLABU za Barcelona na
Real Madrid zinatarajiwa kukutana Desemba katika ratiba mpya ya msimu wa
2016-2017 wa La Liga iliyotolewa leo. Madrid waliomaliza katika nafasi
ya pili katika msimamo wa La Liga nyuma ya Barcelona msimu uliopita,
watasafiri kwenda Camp Nou katika wikiendi ya Desemba 3 au 4 ukiwa ni
mchezo wao wa mwisho kwa la Liga kabla ya kusafiri kwenda kushiriki
michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia nchini Japan wakiwa kama mabingwa wa
Ulaya. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 8 na
kumalizika Desemba 18 mwaka huu. Mechi ya marudiano kati ya mahasimu hao
wa La Liga inatarajiwa kufanyika Santiago Berbabeu kati ya Aprili 22 au
23 mwakani.
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni