KWA hesabu
za harakaharaka, timu ya Yanga imeshatupwa nje ya michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika baada ya kucheza mechi tatu na kufungwa mbili huku ikiambulia
sare moja.
Kwenye kundi
lake, yenyewe ndiyo inaburuza mkia ikiwa na pointi moja iliyoipata juzi
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ilipofungana bao 1-1 na Medeama na
kumaliza mzunguko wa kwanza.
Katika mzunguko huo wa kwanza, Yanga imecheza mechi mbili nyumbani dhidi ya TP Mazembe na Medeama huku moja ikiwa ni ya ugenini ambayo ni dhidi ya MO Bejaia.
Mzunguko wa
pili watacheza mbili ugenini dhidi ya Medeama na TP Mazembe kabla ya
kuwakaribisha MO Bejaia hapa nyumbani.
Kama Yanga inataka kufuzu hatua ya nusu fainali, inahitaji kufanya maombi ili wapinzani wake wateleze kwenye mechi zijazo huku yenyewe ikusanye pointi zote tisa katika mechi zake hizo tatu na kumaliza na pointi kumi.
Kwenye soka
lolote linaweza kutokea lakini kiuhalisia inaonekana ni ngumu kwa Yanga kutoka
mkiani na kutinga nusu fainali ambapo timu mbili kutoka kila kundi ndizo
zitafuzu.
Ukiangalia
kwenye michezo yake ya nyuma, Yanga haikuwa ikifanya vizuri ugenini zaidi ya
kuutumia uwanja wake wa nyumbani ambapo sasa hivi watacheza hapo mechi moja tu
kati ya tatu zilizosalia.
Licha ya
kuonekana kuwa na ugumu, lakini binafsi nawapongeza kwa kufika hapo kwani kwao
ni mafanikio makubwa kutokana na muda mrefu kuishia hatua za mwanzoni.
Kilichobaki
sasa ni kutokata tamaa kwa sababu ukiangalia ukanda mzima wa Afrika Mashariki,
hakuna timu iliyobaki katika michuano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu zaidi ya
Yanga.
Yanga
iliyoanza msimu huu kwa kuiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika
kabla ya kudondokea Kombe la Shirikisho, msimu ujao tena itashiriki Ligi ya Mabingwa
kutokana na kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika Mei, mwaka huu.
Hii ni nafasi nyingine kwao kusahihisha makosa yaliyotokea msimu huu na nadhani kama kweli watakuwa na nia thabiti bila shaka watafanikiwa.
Kuna msemo unasema kuteleza si kuanguka, Yanga inatakiwa kujifunza kwa kile walichokiona msimu huu ili msimu ujao wafikie malengo yao japo nusu yake endapo watashindwa yote.
Yanga
wanatakiwa kufahamu kuwa hakuna timu iliyofanikiwa kimataifa au ngazi yoyote
ile bila ya kupitia misukosuko, hata hizo zinazotesa leo nazo zilikuwa na
wakati mgumu huko nyuma au zingine hata sasa zinakumbana na matatizo licha ya
kuwa na mafanikio.
Licha ya
hivyo, najua wapo waliofurahia kufanya vibaya kwa Yanga kutokana na itikadi zao
kiushabiki, hawapaswi kubadili mawazo yao na waendelee kufurahi ili Yanga
waumie na mwisho wake watafute njia za kuwabadilishia kibao.
Group A
Pos | Team
|
Pld | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | TP Mazembe | 3 | 2 | 1 | 0 | 4 | 1 | +3 | 7 | ||||||
2 | MO Béjaïa | 3 | 1 | 2 | 0 | 1 | 0 | +1 | 5 | ||||||
3 | Medeama | 3 | 0 | 2 | 1 | 2 | 4 | −2 | 2 | ||||||
4 | Young Africans | 3 | 0 | 1 | 2 | 1 | 3 | −2 | 1 |
mdosejr@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni