

Kuingia kwa goli hilo kuliwafanya Medeama kucheza kwa tahadhari kubwa na huku wakimuweka mchezaji mmoja mbele.
Katika dakika ya17 Medeama walifanikiwa kupata goli la kuswazisha kufuatia mpira wa kona uliochezwa na wachezaji wa tatu wa Medeama na kufunga goli hilo kupitia kwa Bernard Danso.
Kuingia kwa gol hilo kuliongeza kasi ya mchezo huku yanga sc wakiendelea upoteza nafasi, wakati Medeam muda mwingi wakiwa nyuma huku wakitumia mipira mirefu katika mashambulizi ya kushtukiza.
Kipindi ha pili hali iliendelea kwa hivyo kwa yanga kwa kuendelea kupoteza nafasi za kupatia goli huku Medeama wakipoteza nafasi mbili walizofanikiwa kutengeneza.
Nafasi za wazi zaidi walizotengeneza Yanga SC ni kiupitia kwa Obrein Chirwa na Amisi Tambwe ambapo kila mmoja alipata fursa ya kukutana uso kwa uso na kipa Medeama na kushindwa kuvuisha mpira kwa kipa huyo aliyeokoa michomo mingi ya yanga hii leo na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Licha ya mabadiriko yaliyofanywa kwa mpigo na Yanga kwa kumtoa Oscar Joshua nafasi ikichukuliwa na Juma Mahadh, Amisi Tambwe na kuingia Haruna Niyonzima haikusaidi timu hiyo kupata alama 3 japo mpira uliongezeka kasi baada ya mabadiriko hayo
Matokeo hayo ya leo yanifanya yanga kuwa wamwisho katika kundi B wakiwa na pointi 1, wakati Medeam wakiwa na pointi 2 na TP Mazembe wakiwa kileleni kwa pointi 6, wakati Mo bejaina wanaocheza na Mazembe kesho wakiwa wa pili kwa pointi 4.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Juma Mahadhi, Kelvin Yondani, Mtogo Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe/Haruna Niyonzima dk na Donald Ngoma.
Medeama FC; Daniel Adjei, Samuel Adade, Moses Sapong, Paul Adoo/Salufu Moro dk62, Daniel Amouah, Kwesi Donsu, Erick Kwakwa, Kwame Boahene, Abbas Mohamed, Bernard Ofori na Enock Atta Agyei/Malik Akowuah dk79.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni