HABARI KUBWA ZA KIMICHEZO BARANI ULAYA
SANCHEZ AMPA WENGER MCHECHETO.
Sanchez alipata majeruhi ya kifundo cha mguu wakati wa michuano ya
Copa America na amekuwa akipatiwa matibabu katika kipindi hiki cha
mapumziko ya kiangazi.
Arsenal wamekuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo
ya nyota wao huyo na kuna hofu anaweza kukosa mwanzo wa msimu ambapo
timu hiyo hiyo itaikaribisha Liverpool katika Uwanja wa Emirates Agosti
14 mwaka huu.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger atataka Sanchez awe fiti
ka ajili ya mchezo huo haswa kutokana na uhaba wa washambuliaji alionao
kutokana na michuano ya Ulaya iliyomalizika hivi karibuni.
Kutokana na
michuano hiyo Olivier Giroud, Mesut Ozil na Aaron Ramsey hawatajiunga na
wenzao kwa mazoezi ya maandalizi msimu mpaka Agosti 8 ikiwa ni siku
saba kabla ya mchezo dhidi ya Liverpool.
RONALDO NDIO MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA KWA KIZAZI HIKI - FERGUSON.
MENEJA wa zamani wa
Manchester United, Sir Alex Ferguson anaamini hamu ya soka aliyonayo
Cristiano Ronaldo inamtenganisha na wote akiwa kama mchezaji bora
duniani kwasasa.
Baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa taji lake la pili
la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka mitatu, Ronaldo
aliiongoza timu ya taifa ya Ureno kutwaa taji la michuano ya Ulaya kwa
kuwafunga wenyeji Ufaransa Juni 10 mwaka huu.
Ferguson ambaye alikuwepo
Stade de France kushuhudia Ronaldo akitwaa taji hilo la Ulaya, hana
shaka kuwa juhudi kubwa alizokuwanazo nyota huyo ndio sababu kubwa ya
mafanikio aliyonayo sasa.
Ferguson mwenye umri wa miaka 74, ambaye
amefanya kazi na Ronaldo kwa miaka sita akiwa na United, amesema uchu na hamu kubwa ya mchezo wa soka aliyonayo Ronaldo ndio inayomfanya kufikia mafanikio hayo hivi sasa.
amefanya kazi na Ronaldo kwa miaka sita akiwa na United, amesema uchu na hamu kubwa ya mchezo wa soka aliyonayo Ronaldo ndio inayomfanya kufikia mafanikio hayo hivi sasa.
Ferguson aliendelea kudai kuwa Ronaldo
amekuwa akijituma kila siku na mara zote amekuwa akitaka kuimarika zaidi
na kushinda haswa katika mechi kubwa.
Kocha huyo mkongwe amesema kwa
kawaida wachezaji wakubwa hucheza kwa kiwango cha juu kwa miaka mitano
au sita tu lakini Ronaldo ni tofauti kwa amefanya hivyo kwa zaidi ya
miaka 10 ndio anadhani ndio mchezaji bora kabisa kutokea katika kizazi
hiki.
MAN UNITED BADO WAMSARANDIA SANCHEZ.
KLABU ya Manchester
United inadaiwa kuwa tayari imeshaiuliza Bayern Munich kuhusu kutenzi
cha kutengua mkataba wa Renato Sanchez.
United walikuwa wakiongoza mbio
za kumsajili chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 mapema mwaka huu
lakini walishindwa mbio hizo na Bayern ambao walimsajili kwa kitita cha
paundi milioni 37.7 kutoka Benfica.
Lakini Mourinho na United
wameonyesha kufurahishwa na kiwango kikubwa alichoonyesha Sanchez wakati
akiitumikia Ureno katika michuano ya Ulaya na sasa wanataka kujulishwa
kuhusu kitenzi chake alichowekewa katika mkataba wake na
Bayern.
Mourinho ambaye pia anamfukuzia Paul Pogba, inadaiwa
ameshangazwa kwa United kuikosa nafasi ya kumsajili Sanchez mpaka
akaenda Bayern.
CHELSEA YATENGA PAUNDI MILIONI 80 KUSAJILI WAWILI KA MPIGO.
KLABU ya Chelsea
inadaiwa kukaribia kuwasajili nyota wawili N’Golo Kante na Kalidou
Koulibaly kwa jumla ya paundi milioni 80.
Kante ambaye amekuwa mmoja
kati ya viungo bora wa Ligi Kuu msimu uliopita wakati Leicester City
walitawadhwa mabingwa, anadaiwa kukaribia kutua Stamford Bridge kwa
kitita cha paundi milioni 30 kiasi ambacho kimekubaliwa na pande zote
mbili.
Kufuatia kumkosa beki wa kati wa Juventus Leonardo Bonucci,
Antonio Conte sasa amegeuzia nguvu zake kwa Koulibali anayayekipiga
Napoli, wakati akijaribu kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Mabingwa hao wa
Serie A wanadaiwa kutaka paundi milioni 50 kwa nyota huyo mwenye umri
wa miaka 25, na pamoja na Everton pia kutajwa kumuwania beki huyo
Chelsea wanaamini wao ndio wenye nafasi kuba ya kumnasa.
MOURINHO KUMUACHA IBRAHIMOVIC ZIARA YA CHINA.
MENEJA mpya wa
Manchester United, Jose Mourinho anafikiria kumuacha Zlatan Ibrahimovic
wakati watakaposafiri kwa ajili ya ziara ya kwenda kucheza mechi mbili
nchini China Jumanne ijayo.
Nyota wa kimataifa wa Uingereza Wayne
Rooney, Chris Smalling na Marcus Rashford wanatarajiwa kuwepo katika
ziara hiyo.
Hata hivyo, Mourinho amesema wachezaji hao hawatacheza
mchezo dhidi ya Borussia Dortmund utakaofanyika jijini Shanghai Julai 22
na ule dhidi ya mahasimu wao Manchester City utakaofanyika jijini
Beijing Julai 25.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 34, yeyey anatarajiwa
kutojumuishwa kabisa katika kikosi hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni