MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga bao lake la kwanza katika michuano ya Europa League usiku huu, timu yake, KRC Genk ikiilaza 2-0 Buducnost ya Montenegro Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya mchujo, Samatta alifunga bao la pili dakika ya 79, baada ya kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Neeskens Kebano kufunga la kwanza kwa penalti dakika ya 16.
Samatta amekata utepe wa mabao Europa League |
Genk sasa itatakiwa kwenda kuulinda ushindi wake katika mchezo wa marudiano Julai 21, Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica ili kusonga mbele Raundi ya Tatu ya mchujo.
Ratiba ya Raundi ya Tatu ya mchujo itapangwa leo na mechi za kwanza zitachezwa Julai 28 wakati marudiano yatakuwa Agosti 4, mwaka huu.
Timu zitakazoshinda zitakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi, ambako sasa vigogo kama Manchester United ya England wataanzia huko.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Castagne, Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Buyens/Heynen dk73, Kebano/Karelis dk76, Bailey, Buffalo na Samatta/Trossard dk87.
Buducnost Podgorica : Dragojevic, Vusurovic (84 'Camaj), Mitrovic, Vukcevic, Radunović, Pejakovic/Seratlic dk74 Raickovic/Janketić dk59, Hoko, Đalović, Mirkovic na Raspopovic
Inawezekana hukuweza kuliona goli lililofungwa na Samatta, hii hapa video ya goli hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni