Mwezi uliopita
Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 136 lakini mwezi huu imepanda na
kushinda nafasi hiyo huku kwa upande wa Afrika ikishika nafasi ya 36
ikizizidi nchi za Burundi iliyopo nafasi ya 125 duniani na 38 Afrika na
Sudan Kusini nafasi ya 153 kwa 47 kwa nchi ukanda wa Afrika
Mashariki.
Nchi inayoongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki ni Uganda
waliopo nafasi ya 69 duniani na 15 Afrika wakifuatiwa na Kenya waliopo
nafasi ya 86 duniani na 22 Afrika na Rwanda ndio wanaoshika nafasi ya
tatu wakiwa katika nafasi ya 111 duniani na 32 Afrika.
Kwa upande wa
Afrika orodha hiyo bado imeendelea kushikiliwa na Algeria ambao wako
nafasi ya 32 duniani wakifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 35,
Ghana nafasi ya 36, Senegal nafasi ya 41 na Misri ndio anakamilisha tano
bora ya Afrika wakiwa nafasi ya 43.
Kwa upande wa orodha za jumla,
Argentina bado wameendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na Ubelgiji katika
nafasi ya pili, Colombia nafasi ya tatu, Ujerumani nafasi ya nne,
mabingwa wa Copa America Chile nafasi ya tano na mabingwa wa Ulaya Ureno
wao wako nafasi ya sita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni