Kocha Hans van der Pluijm akizungumza na kiungo Deus Kaseke mazoezini jana Jangwani |
KIUNGO Deus David Kaseke jana amefanya mazoezi na Yanga baada ya kukosekana kwa wiki tatu kutokana na maumivu aliyopata baada ya ajali ya pikipiki.
Kaseke alikosekana Yanga SC katika mechi zote dhidi ya Medeama ya Ghana Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, wakitoa sare ya 1-1 nyumbani Dar es Salaam na kufungwa 3-1 Ghana baada ya ajali ya pikipiki.
Lakini sasa kiungo huyo amepona majeraha yake naa anajaribu kurejea kwa ajili ya mchezo ujao Agosti 13 dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga wakinywa maji wakati wa mapumziko mafupi jana |
Na
kocha Mholanzi Hans van der Pluijm alilazimika kushuka Jangwani baada
ya jitihada za kupata uwanja wa kukodi kama ilivyo ada yao kugonga
mwamba jana.
Yanga
ilirejea Dar es Salaam Alhamisi usiku ikitokea Ghana ambako Jumanne
ilipigwa 3-1 Medeama katika mfululizo wa mechi za Kundi A Kombe la
Shirikisho.
Na
hicho kilikuwa kipigo cha tatu katika mechi nne, baada ya awali
kufungwa 1-0 mara mbili nyumbani na ugenini, dhidi ya MO Bejaia Algeria
na TP Mazembe Dar es Salaam.
Beki Mtogo mwenye asili ya Ivory Coast, Vincent Bossou akipasha jana |
Hassan Kessy naye ameendelea na mazoezi ingawa hawezi kucheza mashindano haya |
PICHA NA BINZUBEIRY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni