MSHAMBULIAJI wa
Bordeaux, Jeremy Menez amefanyiwa upasuaji baada ya kipande cha sikio
lake la kulia kukatika katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya
dhidi ya Fc Lorient jana.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye
amejiunga na Bordeaux akitokea AC Milan siku tatu zilizopita, alipata
majeruhi hayo kufuatia kugongana kwa bahati mbaya na kiungo wa Lorient
Didier Ndong dakika ya 15 ya mchezo.
Katika taarifa iliyotolewa na
mtandao wa klabu hiyo, Jeremy anadaiwa kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya
kushona sikio lake.
Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa muda wa Jeremy
kurejea uwanjani utategemea jinsi sikio lake litakavyopona.
Bordeaux
ambao walimaliza katika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligue 1 msimu
uliopita, wanatarajia kuanza kampeni zao kwa kupepetana na St Etienne
Agosti 13 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni