NYOTA
wawili wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale watapambana na
Antoine Griezmann wa Atletico Madrid kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa
Mwaka wa Ulaya.
Bodi
ya Soka Ulaya (UEFA) imetangaza orodha fupi ya mwisho ya wachezaji
watatu wa kuwania tuzo hiyo leo na wachezaji wa la Liga watupu
watachuana, tena wote kutoka timu za Jiji la Madrid.
Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana baada ya kupigiwa kura na matokeo yatatangazwa katika Grimaldi Forum mjini Monaco Agousti 25.
Waandishi wa Habari kutoka nchi zote wanachama 55 wa UEFA watawasilisha orodha yao fupi, huku 54 wakipiga kura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni